KATIBU mkuu wa Wizara ya Maji, Prof.
Kitilya Mkumbo, ametangaza rasmi kuanza kufanya kazi rasmi kwa Wakala
wa Usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingiria (Ruwasa) Julai mosi mwaka
huu, huku wananchi wa vijijini wanaofikiwa na huduma ya maji ikifikia
asilimia 64.8.
Profesa Mkumbo, ametangaza hayo leo
Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuanza
kufanya kazi kwa wakala huo na kuhusu mkutano wa Saba wa mwaka wa Bodi
za maji za mabonde utakaofanyika kuanzia Julai 9 hadi 11 mwaka huu
mkoani Kigoma Ujiji.
Amesema mamlaka hiyo imeanza kufanya kazi
rasmi leo july, mosi na itazinduliwa rasmi july 16 mwaka huu, lakini
kuanzia leo itaendelea kufanya kazi kama kawaida, utasaidia sana
utapikanaji wa maji safi na salama kwa maeneo ya vijijini.
Amebainisha kuwa mpaka kufikia Aprili
mwaka huu jumla ya vituo vya kuchotea maji vilikuwa 131370 vilikuwa
vimejengwa vijijini na vilipaswa kuhudumia watu milioni 32.8 sawa na na
asilimia 83 lakini ni vituo 86,700 sawa na asilimia 65.6 pekee ndivyo
vinavyofanya kazi vikihudumia watu milioni 25.3 sawa asilimia 64.8 ya
wananchi washio vijijini.
Profesa Mkumbo amefafanua kuwa hiyo ni
changamoto kubwa na kwamba sekta ya maji vijijini inakabiliwa na
usimamizi hafifu wa maji pamoja nab zingine hali hiyo inasababishwa na
wahandisi maji kuwajibika kwa mamlaka zaidi ya moja na hivyo kutumika
kwa zaidi ya kazi ya ujenzi wa miradi ya maji.
“Ili kukabiliana na changamoto za kimfumo
zinazokabili sekta ya maji nchini Rais Dk John Magufuli Mei 10 mwaka
jana alitoa maelekezo ya kisera kuwa watumishi wote wa sekta ya maji
wahamishiwe Wizara ya Maji ndio tukaamua kuunda mamlaka hii,”amesema.
Amewataja maofisa walioteuliwa kukaimu
nafasi mbalimbali za uongozi wa RUWASA katika ngazi ya kitaifa na mikoa
wameshateuliwa nao ni pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Gonsalves
Rutakyamirwa, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usambazaji maji na usafi wa
Mazingira, Mkama Bwire.
Alibainisha kuwa wengine ni Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi, Deusidet Magoma, Kaimu Mkurungezi wa
Mipango na Uratibu wa CBWSOs Enock Wagala, Kaimu Meneja wa Kitengo cha
Sheria, Gloria Chegeni, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ndani Herieth Kaiza.
Wengine walioteuliwa ni maofisa
watakaokaimu nafasi ya Meneja wa RUWASA katika mikoa na mikoa
waliyopangiwa, ni Joseph Makaidi mkoa wa Arusha, Godfrey Kabula mkoa wa
Dodoma, Nicas Ligombi mkoa wa Geita, Shaban Jellan mkoa wa Iringa,
Sylivester Paulini mkoa wa Katavi, Mathius Mwenda Mkoa wa Kigoma, Frank
Elisa mkoa wa Kilimanjaro, Renatus Gumba mkoa wa Lindi.
Kwa upande wa mkoa wa Manyara
aliyeteuliwa ni Mary Mbowe, mkoa wa Mara Muhibu Lubasa, mkoa wa Mbeya
Mathayo Athmani, mkoa wa Morogoro Emmanuel Alexandar, mkoa wa Mtwara,
Mbaraka Ally, mkoa wa Mwanza Warioba Sanya na Frederick Magige mkoa wa
Njombe.
Wengine kuwa, mkoa wa Pwani Beatrice
Kasimbazi, mkoa wa Rukwa Shaaban Daud, mkoa wa Ruvuma Hans Nestory, mkoa
wa Shinyanga Julieth Mganga, mkoa wa Simiyu Hatari Kapufi, mkoa wa
Singida Genes Kimaro, mkoa wa Songwe Pambe Pambe, mkoa wa Tanga John
Msengi na Mariam Majala mkoa wa Tabora.
Profesa. Kitila alisema tayari
wameshateua majina katika mikoa 24 na kwamba umebaki mkoa mmoja wa
Kagera bado hawajateua na atateuliwa baadaye.
Aidha ametumia nafasi hiyo kutangaza
mkutano mkuu wa Saba wa Bodi za Maji za Mabonde, kuwa utafanyika katika
mkoa wa Kigoma Ujiji, utakao kuwa na kauli mbiu ni Rasilimali za Maji
ni Msingi wa Maendeleo Endelevu ambayo inalenga kuonesha uhusiano mkubwa
uliopo kati ya uwepo wa rasilimali za maji na maendeleo ya nchi pamoja
na ustawi wa jamii.
“Katika mkutano huo utakaofanyikia ukumbi
wa NSSF Manispaa ya Kigoma Ujiji, mgeni rasmi atakuwa waziri wa Maji
Profesa Makame Mbarawa, mwenyeji wa mkutano huo atakuwa Bodi ya Maji ya
Bonde la Ziwa Tanganyika ambayo makao yake makuu ni Kigoma,amesema prof
Mkumbo.
Pamoja na umuhimu na kazi kubwa ya
kusambaza maji, kazi hiyo ni ya muda mfupi na itafikia wakati
itakamilika lakini changamoto za maji ili kujihusishia usalama wa maji
kwa ajili ya matumizi mtambuka.
0 comments:
Post a Comment