METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, July 19, 2019

MHE.AWESO ATOA MAELEKEZO MRADI WA MAJI MASANGE WILAYANI KONDOA

Naibu Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Masange wilayani Kondoa baada ya kufanya ziara ya kukagua na kujionea mradi wa maji.

Mbunge wa Jimbo la Kondoa vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dokta.Ashatu Kijaji,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Masange wilayani Kondoa wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso alipofanya  ziara ya kukagua na kujionea mradi wa maji.

Mwenyekiti wa Maji Kijiji cha Masange Bw.Bakari Mnyoti ,akitoa kero yake kwa Naibu Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso (hayupo pichani) ambapo alifanya ziara ya kukagua na kujionea mradi wa maji.

Mkazi wa Kijiji cha Masange Bi.Mariam Isaka ,akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso (hayupo pichani) ambapo alifanya ziara ya kukagua na kujionea mradi wa maji.

Sehemu ya wanakijiji wa Masange wakimsikiliza Naibu wa Maji Mhe.Juma Aweso (hayupo pichani) akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya kukagua na kujionea mradi wa Maji uliopo wilayani Kondoa.

Naibu Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso,akiongozana na baadhi ya wanakijiji na viongozi kupanda mlima kwenda kujionea Taki la Maji ambalo hutumika kusambaza maji katika kijiji cha Masange wilayani Kondoa.

Naibu Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso ,akiwa amepanda juu ya Taki la Maji akikagua na kujionea hali halisi ya maji ya usambazajwi katika kijiji cha Masange.

Mbunge wa Jimbo la Kondoa vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dokta.Ashatu Kijaji,akiongozana na Naibu Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso kupanda juu ya Taki la maji kujionea jinsi maji yanayotumika kusambazwa kwa wanakijiji wa Masange wilayani Kondoa.

…………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Naibu Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amesema Wizara yake itashirikiana na TAKUKURU ili kujiridhisha katika utekelezaji mradi wa Maji katika kijiji cha Masange Wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

Naibu Waziri Aweso ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa eneo hilo alipofanya ziara ya kukagua na kujionea mradi wa Maji kijiji cha Masange uliogharimu kiasi cha Sh.Milioni 433 baada ya kupewa majibu yasiyojitosheleza na Mkandarasi wa Mradi huo.

“Haiwezekani tukauziwa mbuzi kwenye gunia,lazima kukagua na kujionea,baada ya kupewa majibu ya kusuasua hivyo TAKUKURU tutashirikiana nao kubaini ubadhilifu,na mkandarasi asilipwe mpaka tufanye uchunguzi tujiridhishe”amesema Aweso

Hali hiyo imekuja baada ya Mkandarasi wa mradi huo wa Maji kampuni ya Best One kwa kushirikiana na wataalam wa sekta ya Maji wa halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kutoa majibu yasiyoridhisha kuhusu matumizi ya fedha zilizotumika katika mradi huo .

Akijibu kero ya wananchi hao kuhusu Maji Mhe Aweso amepiga simu mbele ya wananchi kwa wataalamu wa Wizara kuulizia taratibu za upatikanaji wa Gari la kuchimba visima katika kijiji hicho ambapo ameahidi kuchimbwa visima viwili kwenye Kijiji hicho ndani ya kipindi cha muda mfupi.

Katika kujiridhisha na mradi huo Mhe Aweso alilazimika kupanda kwenye mlima ambao chanzo cha maji kinapatikana ambapo alikiri kuwepo kwa changamoto Na kuahidi kuzimaliza ili wananchi wa Masange waweze kupata maji na kwenda sawa na kauli mbiu ya kumtua mama ndoo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kondoa vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dokta.Ashatu Kijaji amesema yupo tayari kufanya kazi hata saa sita usiku na walichomwagiza wananchi wake ni kutatua kero ya Maji .

Dkt.Kijaji amesema kuwa wananchi wa Mtaa wa Masange wamesema adha kubwa inayowakabili ni maji hivyo ni vyema serikali ikafanya mchakato haraka kutatua kero hiyo.

Awali ,akisoma taarifa ya Mradi wa Maji wa Masange mbele ya Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso,Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji vijijini[RUWASA]Wilaya ya Kondoa Mhandisi Falaura Seleman Kikusa amesema mradi wa Maji Masange ulianza tangu tarehe 15,Disemba,2014 na kuzinduliwa rasmi tarehe 13,Septemba ,2016 kupitia mbio za Mwenge wa Uhuru huku ukigharimu zaidi ya Tsh.Milioni 433 .

Aidha amebainisha kuwa muda wa utekelezaji wa Mradi huo kwa mujibu wa Mkataba ni kipindi cha miezi mine kuanzia tarehe 15,Disemba,2014,hadi 15,Machi,2015 hivyo kutokana na changamoto mbalimbali hususan kuchelewa kwa malipo ya madai ya mkandarasi,mradi uliongezewa muda wa utekelezaji na kukamilika rasmi mnamo tarehe 7,Juni,2018.

Mhandisi Kikusa ameendelea kufafanua kuwa upatikanaji wa Maji katika kijiji cha Masange haukidhi mahitaji halisi ya maji kwa wakazi wa kijiji hicho kwani huduma ya maji imekuwa ikipatikana kwa mgao kwa vitongoji kwa masaa manne hadi matano.

Amesema chanzo cha kuwepo kwa hali hiyo unatokana na changamoto kadhaa ikiwemo kuongezeka kwa wakazi pamoja na kukua kwa mji wa Masange ,Uwezo wa chanzo cha Maji [lita 119,577.6 kwa siku]kuwa mdogo ikilinganisha na mahitaji halisi ya Maji ya sasa [zaidi ya lita 141,560 kwa siku] na changamoto nyingine ni usimamizi usio mzuri kutoka kwa timu ya mhandisi.

Hata hivyo mkandarasi wa mradi hadi kufikia sasa alishalipwa kiasi cha sh.347,421,000 kati ya gharama 433,288,548 na zilizobaki kwa mujibu ya makubaliano ya mkataba ni Tsh.120,609,648.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com