Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji na Kata ya Nyimbili wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo ikiwemo matumizi ya fedha za mfuko wa Jimbo la Vwawa tarehe 27 Julai 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ndolezi Kata ya Mlangali wakati wa mkutano wa hadhara akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo tarehe 27 Julai 2019.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji na Ndolezi kilichopo kata ya Mlangali wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo ikiwemo matumizi ya fedha za mfuko wa Jimbo la Vwawa tarehe 27 Julai 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Songwe
Mbunge wa
Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga
akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo ikiwemo matumizi ya
fedha za mfuko wa Jimbo la Vwawa amewaeleza wananchi mambo manne ya muhimu
ambayo yamefanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe
Magufuli katika kipindi cha muda mfupi tangu aingie madarakani Octoba 2015.
Mambo
hayo muhimu aliyowaeleza wapiga kura wake ni pamoja na Ujenzi wa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme katika Mto
Rufiji.
Alisema
kuwa Mradi huo unajengwa kwa fedha za ndani upo katika eneo la Selous
ambalo ni moja ya maeneo ya turathi za dunia, Mradi huo ambao unafahamika
pia kwa jina la Stieglers Gorge, unatazamiwa kuzalisha megawati 2,000 za umeme,
hatua ambayo ameeleza kwamba itasaidia kupunguza tatizo la nishati hiyo muhimu
kiuchumi na kijamii. Hivyo Tanzania kuwa na utoshelevu wa umeme.
Mhe
Hasunga ameeleza pia kuhusu Ujenzi wa reli ya kisasa, ambapo alisema kuwa nchi nyingi zilizoendelea duniani zinatumia reli kuchochea
ukuaji uchumi na biashara kwa sababu usafirishaji kwa kutumia njia hiyo una
uwezo wa kubeba mizigo mikubwa kwa mara moja na kwa gharama nafuu kulinganisha
na aina nyingine za usafirishaji.
Alisema,
Serikali imedhamiria kujenga Reli ya Kisasa (SGR) kwa kiwango cha kimataifa na
Shirika la Reli Tanzania (TRC) ndilo limepewa dhamana ya kusimamia mradi huo.
Reli inayojengwa (Standard Gauge), yenye upana wa mita 1,435 ndio mfumo
unaotumika sasa ukikadiriwa kuchukua asilimia 50 ya mitandao ya reli duniani.
Katika
mikutano yake zaidi ya 24 aliyoifanya katika Jimbo hilo kwa takribani siku nne
Mhe Hasunga ametaja pia juhudi za Rais Magufuli kwa kuamua kununua Ndege zaidi
ya nane.
Alisema kuwa Miaka ya nyuma Kabla ya Rais wa Tanzania aliyopo sasa
madarakani Dkt John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais, Shirika la ndege nchini
Air Tanzania lililoanzishwa tangu Mwaka 1977 lilikuwa na Ndege moja aina ya
Bombardier DASH8 Q300 ambayo ilikuwa ikihudumu tangu 2011. Baada ya Rais
Magufuli kuingia madarakani Mwaka 2015 na kuanza mkakati wa kulifufua Shirika
hilo na kuonesha nia ya kununua ndege mpya za Tanzania.
Kuna Bombardier DASH8 Q400 tatu, mbili ambazo
zilifika Tanzania Septemba 2016 na moja Juni 2017; Bombardier CS300 mbili na
Boeing 787 Dreamliner ambazo zilitua Tanzania kati ya mei na Julai 2018. Ndege
nyengine ni Airbus A220-300
Alisema
ununuzi wa ndege hizo ni mkakati muhimu wa serikali inayotekeleza ilani ya
uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 ni sehemu ya kurahisisha
usafirishaji wa mazao ya Kilimo hivyo kuboresha sekta ya Kilimo sambamba na
kuinua kipato cha wananchi kwani mazao mengi yanaoza shambani lakini kupitia
usafirishaji huo mazao yote yatakuwa na tija.
Jambo la
nne ni kuhusu Elimu bure, Waziri Hasunga alisema kuwa Katika kipindi cha muda
mrefu Tanzania kulikuwa na wimbi la wanafunzi kushindwa kuendelea na masomo
kutokana na wazazi/walezi kukosa fedha za kuwalipia ada. Katika kuliona hilo
Rais Magufuli aliamua kufuta ada kuanzia elimu ya awali hadi sekondari, jambo
ambalo limeongeza idadi ya wanafunzi ambao wamejitokeza kusoma.
Alisema
kuwa maono ya Rais Magufuli yamezaa matunda kwani wananchi wengi sasa watoto
wao wananufaika na serikali yao kwani imekuwa mkombozi katika sekta ya elimu.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment