Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Wafanyabishara Wanawake wa
Masokoni na Wananchi wa Dodoma kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa
kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na
Watoto katika maeneo ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019
katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na
Wafanyabishara Wanawake wa Masokoni na Wananchi wa Dodoma kwenye Hafla
ya Uzinduzi wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na
Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko. Hafla
hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square
Jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata Utepe kuzindua rasmi Mradi wa
kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake
na Watoto katika maeneo ya Masoko pamoja na ugawaji wa Pikipiki 14 kwa
Maafisa wa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino
Dodoma kwa ajili ya kuongeza kurahisisha Usafiri katika kufanikisha
kutokomeza Ukatili na Unyanyasaji kwa Wanawake na watoto . Hafla hiyo
imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini
Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akionesha Bango Juu kama ishara ya
Uzindua rasmi Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na
Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko pamoja
na ugawaji wa Pikipiki 14 kwa Maafisa wa Maendeleo ya Jamii wa
Halmashauri ya wilaya ya Chamwino Dodoma kwa ajili ya kuongeza
kurahisisha Usafiri katika kufanikisha kutokomeza Ukatili na Unyanyasaji
kwa Wanawake na watoto . Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika
Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. Katikati Mwenyekiti wa ALAT
Taifa na Meya wa Manispa ya Shinyanga Mhe. Gulamhafeez Z. Mukadam na
Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Funguo ya Pikipiki Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith S. Mahenge Baada ya kuzindua rasmi Mradi
wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya
Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko kwa ajili ya kuongeza Chachu
ya kurahisisha Usafiri katika kufanikisha zoezi hilo, Jumla ya Pikipiki
14 zilitolewa kwa Mkoa wa Dodoma . Hafla hiyo imefanyika leo Julai
30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Bidhaa mbalimbali
zinazotengenezwa na Wajasiriamali Wanawake katika Mkoa wa Dodoma
alipotembelea Mabanda ya Maonesho kwenye Uzinduzi wa Mradi wa kutokomeza
vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto
katika maeneo ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika
Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Masokoni
Wanawake na Wanancho wa Dodoma, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akihutubia
kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji
na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko.
Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere
Square Jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mratibu wa Umoja wa
Mataifa Tanzania Alvaro Rodriquez walipokutana kwenye Hafla ya Uzinduzi
wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya
Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo
Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa
kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Usawa wa Kijinsia na
Uwezeshaji wanawake (UN WOMEN) Bibi. Hadon Addou walipokutana kwenye
Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na
Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko. Hafla
hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square
Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa ALAT Mhe Gulamhafeez
Mukadam,akizungumza na Wafanyabishara Wanawake wa Masokoni na Wananchi
wa Dodoma kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya
Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo
ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya
Nyerere Square Jijini Dodoma.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
…………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan
amezindua mradi wa kutokomeza vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji
dhidi ya Wanawake na Watoto kwenye masoko na kushauri elimu iendelee
kutolewa kupitia mikutano ndani ya Mitaa na Kata.
Hayo ameyasema leo jijini Dodoma wakati
wa uzinduzi huo ambapo amesema katika kupambana na vitendo hivyo vya
kikatili Serikali imeimarisha utendaji wa madawati 417 ya jinsia na
watoto yaliyopo katika vituo vya Polisi nchini kwa lengo la kuwezesha
huduma stahiki kwa watu wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia.
Mama Samia ameitaka Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Ofisi ya
Rais-TAMISEMI kushirikiana na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ambao ndio
waratibu wa mradi huo katika kuhakikisha afua zinazotekelezwa kupitia
mradi huo zinakua endelevu hata pale utekelezaji wa mradi unapofikia
mwisho.
” Ndugu zangu kila mmoja wetu ana haki ya
kupinga na kutokomeza ukatili wa kijinsia, hivi vitendo havikubaliki na
wala haviruhusiwi kisheria. Yeyote atakayethubutu kumdhalilisha
mwanamke au mtoto tutamchukulia hatua kali.
” Ni jambo la aibu kuona tunatumia viungo
vya wanawake kama matusi, huyu mwanamke unayemdhalilisha tukumbuke ni
kama mama zetu majumbani mwetu, hatuwezi kuwa na Taifa lenye amani kama
tutaruhusu vitendo hivi, tuungane katika kupiga vita na kutokomeza
ukatili wa kijinsia, ” amesema Mama Samia.
Akizungumzia ombwe la watoto wadogo
kufanya biashara kwenye masoko, Mama Samia amezitaka kamati za masoko
kuhakikisha zinashirikiana na mamlaka husika katika kuzuia watoto
kufanya biashara sokoni na badala yake wawahimize kwenda shule na
kuwaripoti wazazi wanaowatuma watoto wao kufanya biashara.
” Serikali yenu ya awamu ya tano
iliwaahidi elimu bure kwa shule ya msingi hadi kidato cha nne. Tunapoona
watoto wetu hawaendi shule na wanafanya biashara sokoni tunakua
hatumtendei haki Rais wetu Dk John Magufuli kwa zawadi ya elimu bure
aliyotuletea. Tuwazuie watoto kufanya biashara sokoni na tushirikiane
kuwapeleka shule,” amesema Mama Samia.
Aidha katika kutekeleza mradi huo, Mhe
Makamu wa Rais amekabidhi Pikipiki 14 kwa ajili ya wataalam wa Maendeleo
ya Jamii wa Mkoa wa Dodoma kwa Kata za Halmashauri ya Chamwino na
kuielekeza Wizara kuendeleza utaratibu huo wa kupatia wataalamu hao
usafiri ili iwe rahisi kwao kuwafikia wanawake wengi hususani wa
vijijini na kuwaunganisha na fursa za kiuchumi.
Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu amemshukuru Makamu
wa Rais kwa kuzindua mradi huo ambao utakua msaada mkubwa katika
mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.
” Mhe Makamu wa Rais kama Wizara
tumejipanga katika kuhakikisha tunaongeza elimu zaidi kwa wananchi iki
tuzidi kupunguza wimbi la vitendo hivi, lengo letu ni kutokomeza kabisa
vitendo hivi ili kuwa na Taifa imara ambalo litakua na mshikamano na
amani baina yetu bila kujali huyu ni Mwanaume au Mwanamke,” amesema
Waziri Ummy.
Nae Mwenyekiti wa ALAT Mhe Gulamhafeez
Mukadam amesema kuna changamoto kwenye dira ya pamoja juu ya utokomezaji
wa vitendo vya ukatili wa kijinsia jambo ambalo linaleta athari ya
maendeleo ya wanawake na hivyo kuzorotesha uchumi wa Nchi.
” Nimpongeze Mkurugenzi wa Jiji la
Dodoma, Mhe Godwin Kunambi kwa namna ambavyo amekua msaada kwa akina
Mama wa Jiji hili kwa kuwapatia mikopo inayowawezesha kufanya biashara
zao. Serikali za Mitaa jukumu lao ni kuwawezesha wananchi wao kuzipata
fursa.
” Lakini pia kuna changamoto ya masoko,
lugha chafu kwa wanawake sokoni hizi changamoto zinapaswa kushughulikiwa
na kutokomezwa kabisa. Tukiwawezesha wanawake na kuwaepusha na vitendo
vya unyanyasaji tutakua tunatengeneza Taifa imara na madhubuti na kuweza
kufikia azma ya Mhe Rais ya uchumi wa kati kupitia viwanda,” amesema
Mhe Mukadam.
0 comments:
Post a Comment