METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, July 22, 2019

MAGARI YAGONGANA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU 4 ,MAJERUHI 12 KAHAMA

Watu wanne wamefariki dunia na wengine 12 wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea jana majira ya saa mmoja usiku    katika eneo la nyambula kata ya Ngogwa Wilayani  Kahama mkoani Shinyanga baada ya gari aina ya Totoya hice yenye namba za usajili T 710  AZZ na Gari aina ya Land cruiser  yenye namba za usajili T 477 ATC.

Mpekuzi Blog  imezungumza na kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga (ACP) Richard Abwao ambaye alikuwa katika hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama kuhusiana na tukio hilo na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa hice iliyokuwa na abiria ikitokea kakola kwenda kahama.

Amesema barabara ya kakola kahama imekuwa na  vumbi nyingi kutokana na kutumika na magari mengi baada ya kuibuka kwa machimbo mapya ya kakola namba 9 na kuwataka madereva wote kuchukua tahadhari kwa kutoendesha kwa mwendo kasi ili kuzuia ajali.

Amefafanua kuwa leo RTO atakuwa na operation maalum katika barabara hiyo ili kubaini madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani pamoja na kuyaondoa magari mabovu yote barabarani.

Kamanda Abwao Amesema leo  atatoa taarifa rasmi  za ajili hiyo ikiwemo majina ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia leo.

Boniface Makoye shuhuda wa tukio hilo amesema baada ya ajali hiyo kutokea abiria wengi walijeruhiwa na aliweza kuwaokoa baadhi yao ambao walikuwa wamenaswa na vyuma katika hice hiyo.

Taarifa kamili zaidi kuhusiana na ajali hii endelea kufuatilia

Wazo-huru blog

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com