METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, July 12, 2019

JESHI LA POLISI DODOMA LAFANYA MSAKO NA KUKAMATA MAWAKALA HEWA 47 ,LAINI ZA SIMU 4667

Na.Alex Sonna,Dodoma.

  Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma  kwa Kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania [TCRA]   kwa kanda ya kati limefanya Operesheni Maalum ya kuwasaka watu wanaojihusisha na usajili wa laini za simu bila idhini ya makampuni husika ya Simu na kukamata mawakala hewa 47 na laini za simu 4667..

Akizungumza  na Waandishi wa Habari jijini Dodoma , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gillese Muroto amesema katika Msako huo umehusisha maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma  yakiwemo Majengo,Sabasaba,Mipango,Nyerere Square,Sokoni,St.John , Chang,ombe ,Nanenane, na Nkuhungu,Bahi ambapo wamekamata wanaume 38 na wanawake 9 jumla yake 47.

Kamanda  Muroto amesema katika Msako huo  wamekamata vielelezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na laini za  simu ambapo Vodacom 1300,tigo 1808,Airtel 716 ,Hallotel 694,TTCL 144   ikiwa ni jumla ya laini 4667 pamoja na simu 50 zilizokuwa zikitumika katika usajili huku pia jeshi hilo likibaini makosa ya kitambulisho kimoja kutumika kusajili laini zaidi ya Mtu  mmoja ambapo ni makosa kisheria.

Hata hivyo,Kamanda Muroto ametoa wito kwa Waandishi wa Habari kuendelea kuelimisha jamii juu ya Masuala  ya usajili ili wananchi waweze kuelewa juu ya mawakala matapeli wanaoweza kuiba nyaraka na taarifa muhimu za mawasiliano na utambuzi ikiwani pamoja na vitambulisho.

Kwa Upande wake  Mwakilishi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania[TCRA]kanda ya kati amelishukuru jeshi hilo kwa ushirikiano huku akitoa  wito kwa makampuni ya simu husika kukaa makini juu ya usajili wa laini za simu katika kupambana na wahalifu.

Msako huo ulilenga  kukamata Mawakala wasio kuwa na barua  rasmi kutoka kampuni husika ya simu,msajili alisiyekuwa na ofisi anuani na makazi ya Kudumu,asiyekuwa na leseni ya biashara au vitambulisho vya biashara vilivyotolewa na Rais John Pombe Magufuli.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com