Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa
Aweso,akizungumza katika kikao kazi cha Mameneja wa Mikoa na Wilaya wa
Wakala wa Majisafi, Usafi na Mazingira Vijijini leo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof
Kitila Mkumbo ,akizungumza na Mameneja wa Mikoa na Wilaya wa Wakala wa
Majisafi, Usafi na Mazingira Vijijini katika kikao kazi kilichofanyika
jijini Dodoma.
Sehemu ya Mameneja wa Mikoa na Wilaya wa
Wakala wa Majisafi, Usafi na Mazingira Vijijini wakifatilia kikao kazi
kilichofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa
Aweso,akiwa katika picha ya pamoja na Mameneja wa Mikoa na Wilaya wa
Wakala wa Majisafi, Usafi na Mazingira Vijijini baada ya kumaliza kikao
kazi kilichofanyika leo jijini Dodoma.
………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso
amewataka Mameneja wa Mikoa na Wilaya wa Wakala wa Majisafi, Usafi na
Mazingira Vijijini kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha wanaondoa
changamoto za Maji katika maeneo yao.
Mhe Aweso ameyasema hayo wakati
alipokutana na Mameneja hao jijini Dodoma ambapo amesema kwa sasa Wizara
hiyo imeunda kitengo cha usanifu ambacho kitasaidia katika kuangalia
upya usanifu, mikataba na gharama zinazowekwa na wakandarasi kabla ya
ujenzi wa miradi.
Amewataka Mameneja hao kutumia weledi na
taaluma zao kuhakikisha wanamtua mama ndoo kichwani na kuwataka kuacha
mambo ya hovyo yaliyokuepo awali.
” Katika ziara zangu zote katika maeneo
mbalimbali nimekua mkali sana kwa wahandisi na wakandarasi, baadhi ya
wataalamu wametuangusha kwa kutumia miradi kujipatia fedha, nimejionea
mwenyewe miradi mingi wakishindwa kuimaliza kwa wakati. Wakandarasi hawa
hatuwezi kuwavumilia hata kidogo.
” Mhe Rais ametuamini sana katika nafasi
hizi tulizoteuliwa, ni jukumu letu kumsaidia kazi na kutumia taaluma
zetu kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa wananchi waliopo vijijini
inafikiwa kwa asilimia 85 au zaidi ifikapo mwaka 2020,” amesema Mhe
Aweso.
Amewataka Mameneja hao kutosubiri Waziri
au Katibu Mkuu kufika katika maeneo yao ya kazi na kuwaonesha changamoto
badala yake waunde mikakati ya kuwawezesha kufikia maeneo yenye
changamoto ya Maji ili waweze kuitatua.
Awali akimkaribisha Naibu Waziri, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof Kitila Mkumbo amesema malengo ya Wizara
hiyo ni kuongeza upatikanaji wa Maji kufikia asilimia 84 kutoka asilimia
64 kwa maeneo ya Vijijini, lakini pia wakifikia asilimia 95 kutoka
asilimia 84 kwa maeneo ya Mjini.
” Tumekua tukiwekeza sana kwenye miradi
mipya lakini kama tukiongeza nguvu na kumaliza miradi ambayo
imekwishaanza na kuanza kufanya basi tungekua mbali sana hivyo katika
bajeti zetu lazima tupange bajeti zetu Katika kukarabati miradi ya
zamani.
” Mhe Naibu Waziri kazi kubwa na ya
haraka kufanywa na RUWASA ni kujenga imani kubwa kwa Mhe Rais na
Wananchi, na imani hiyo itajengwa na wahandisi hawa kwa kuhakikisha
miradi ya wananchi inafanya kazi lakini kubwa zaidi ni kumaliza tatizo
la Maji,” amesema Prof Mkumbo.
0 comments:
Post a Comment