Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew John Mtigumwe
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew
John Mtigumwe anautangazia Umma wa watanzania kwamba Wizara ya Kilimo ipo
kwenye mchakato wa maboresho ya Sera ya Taifa ya Kilimo ya Mwaka 2013.
Maboresho haya yanalenga kuhuisha shughuli za kilimo ili ziendane na mahitaji
halisi ya nchi ikiwa ni pamoja maendeleo ya viwanda.
Timu ya Wataalam ya Wizara ya Kilimo
inaendelea na ukusanyaji wa maoni kutoka kwa Wadau maeneo mbalimbali ya nchi
ikizingatia pia ushiriki wa makundi mbalimbali ya Kijamii.
Ili kutoa fursa kwa kila Mwananchi. Wizara
inatoa wito kwa Wadau wote hasa wanaojihusisha na shughuli za kilimo, kutoa
maoni, ushauri na michango yao na kushiriki katika mikutano hiyo; au kwa kupiga
simu, kuandika barua na barua pepe kwa anwani zifuatazo:-
Katibu Mkuu,
Wizara ya Kilimo,
S.L.P 2182
40487 DODOMA.
Barua pepe: ps@kilimo.go.tz na
dpp@kilimo.go.tz
Simu: 022-26 2321407
Tarehe ya mwisho ya kutoa maoni ni: -
30.06.2019
Taarifa hii imetolewa na:-
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
WIZARA YA KILIMO,
DODOMA,
04.06.2019
0 comments:
Post a Comment