METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, June 6, 2019

WAFUNGWA MASHABIKI WA SIMBA WAWALAZA WENZAO WA YANGA 1-0 ‘MAVUNDE AKABIDHI KOMBE NA MPIRA’

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Antony Mavunde,akizungumza na uongozi wa Gereza la Msalato kabla ya kukabidhi jezi kwa timu ya wafungwa Mashabiki wa Simba na Yanga

Timu za wafungwa wa Mashabiki wa Simba na Yanga zikiingia uwanjani kupasha misuli kabla ya mechi kupiga ambapo Mashabiki wa Simba wamewalaza wenzao wa Yanga 1-0 katika Gereza la Msalato lilipo jijini Dodoma

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Antony Mavunde,akikagua timu zote mbili za wafungwa Mashabiki wa Simba na Yanga katika Gereza la Msalato kabla ya mpira kuanza.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Antony Mavunde,akitoa neno kwa timu zote mbili za wafungwa Mashabiki wa Simba na Yanga katika Gereza la Msalato kabla ya mpira kuanza.

Kikosi cha Timu ya wafungwa wa Mashabiki wa Simba wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya Mechi yao na wenzao wa Yanga iliyopigwa uwanja wa Gereza la Msalato lililopo jijini Dodoma.

Kikosi cha Timu ya wafungwa wa Mashabiki wa Yanga wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya Mechi yao na wenzao wa Simba iliyopigwa uwanja wa Gereza la Msalato lililopo jijini Dodoma.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Antony Mavunde,akiingia uwanjani tayari kwa kufungua uzinduzi wa mechi kati ya wafungwa Mashabiki wa Simba na Yanga katika Gereza la Msalato kabla ya mpira kuanza.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Antony Mavunde,akipiga Penalti kwa kuashiria pambano la Mpira kati ya wafungwa wa timu za Mashabiki wa Simba na Yanga katika Gereza la Msalato kabla ya mpira kuanza.

Matukio katika picha timu zote mbili za wafungwa Mashabiki wa Simba na Yanga wakichuana vikali Mechi ambayo imepigwa katika uwanja wa Gereza Msalato jijini Dodoma ambapo Mashabiki wa Simba wameibuka washindi wa goli 1-0.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Antony Mavunde,akiwa Meza Kuu na baadhi ya Viongozi akishuhudia Mpira wa Miguu kati ya wafungwa Mashabiki wa Simba na Yanga katika Gereza la Msalato ambapo Timu ya Mashabiki wa Simba wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenzao wa Yanga.

Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini Mh.Antony Mavunde,akikabidhi zawadi ya dawa ya meno kwa Nahodha wa Kikosi cha Timu ya Wafungwa wa Mashabiki wa Yanga katika mechi ambapo Mashabiki wa Simba wameibuka Kidedea kwa ushindi wa bao 1-0 katikati ni Mbunge wa viti maalum Mariam Ditopile

Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini Mh.Antony Mavunde,akikabidhi ya Kombe pamoja na Mpira kwa Nahodha wa Kikosi cha Timu ya Wafungwa wa Mashabiki wa Simba katika mechi ambapo Mashabiki wa Simba wameibuka Kidedea kwa ushindi wa bao 1-0 katikati ni Mbunge wa viti maalum Mariam Ditopile.

Picha na Alex Sonna-Wazo huru blog


………………..

Na.Alex Mathias,Dodoma

Timu ya wafungwa mashabiki wa Simba katika Gereza la Msalato Jijini Dodoma imeibuka na Ushindi wa 1-0 dhidi ya timu ya Mashabiki wa Yanga mchezo uliopigwa katika uwanja wa Gereza hilo ukihudhuliwa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa kanda hiyo.

Mechi hiyo iliyochezwa katika sikukuu ya Idd pili ikiwa ni hitimisho la Bonanza lililoandaliwa na Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini Mh.Antony Mavunde ilianza majira ya saa sita kamili za Mchana,

Timu zote zilianza kwa kushambuliana kwa kasi kubwa katika dakika ya 30 timu ya mashabiki wa Simba wakikosa Penalti baada ya mpigaji kupiga shuti nje ya goli.

Mnamo dakika ya 35 mshambuliaji wa timu ya mashabiki wa Simba,Maneno Mwang,ona aliwanyanyua mashabiki wake kwa kufunga bao safi kwa mpira wa Faulo ulioenda moja kwa moja na kumshinda mlinda mlango wa Yanga.

Hadi timu zikienda katika mapumziko Mashabiki wa Simba walikuwa wanaogoza bao 1-0 kwa bila.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote mbili kufanya mabadiliko ambayo yaliwasaidia zaidi Mashabiki wa Simba kulinda bao lao.

Mnamo dakika ya 80 timu ya Mashabiki wa Yanga walikosa Penalti baada ya kuchezaji wao kupiga nje ilitokana na beki wa Simba kumchezea Rafu  na mwamuzi kuamua kuwa tuta hata hivyo alikuzaa matunda.

Hadi Mwamuzi anapuliza kipyenga cha mwisho timu ya Mashabiki wa Simba wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani zao Yanga.

Kwa Ushindi huo Timu ya Mashabiki wa Simba wametwaa ubingwa wa bonaza hilo na kukabidhiwa zawadi mbalimbali  wamekabidhiwa  kutoka kwa Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Antony Mavunde.

Mhe.Mavunde alikuwa mgeni rasmi wa Bonanza hilo,kwa pamoja amekabidhi   zawadi ya Jezi kwa timu zote mbili,sabuni,dawa ya Meno pamoja na Kikombe kwa Timu iliyoshinda ambapo pia ametoa rai kwa watanzania wote kujenga utamaduni wa kuwasaidia watu wenye uhitaji ikiwemo wafungwa kwani ni moja ya sadaka.

“Nitoe wito kwa watanzania wote hasa katika sikukuu hizi,kujenga utamaduni wa kuwasaidia watu wenye uhitaji kama hawa,kwani hiyo ni moja wa Sadaka,watu hawa japo ni wafungwa lakini jamii bado inawahitaji,nami nitaendelea kuja kwa kadri ntakavyohitajika”amesema Mavunde

Kwa upande wao uongozi wa Gereza hilo wao wamekiri kufarijika na kumshukuru Mbunge Mavunde pamoja na wabunge wote kwa ujumla waliojitolea kuwapeleka vitu mbalimbali wakati wote wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com