*********************************************
Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi leo tarehe 10
Juni 2019 amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere
Joseph Butiku kujadiliana masuala mbalimbali ikiwemo namna Wizara hiyo
itakavyoshirikiana na Taasisi ya Mwalimu Nyerere katika maeneo
yanayohusu wananchi.
Katika
mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisi za Wizara zilizopo eneo la Mtumba
jijini Dodoma, Butiku alitumia fursa ya kukutana na Waziri Lukuvi
kumuelezea kazi za taasisi yake hasa katika kushughulikia Amani, Umoja
na Maendeleo ya watu.
Pia
Mkurugenzi huyo wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere alimueleza Lukuvi kuhusu
ufunguzi wa Jengo la Taasisi yake la Ghorofa 30 liliko Dar es Salaam
ambalo linatarajiwa kufunguliwa mwanzoni mwa mwezi
Agosti 2019 ambapo uzinduzi wake utaenda sambamba na sherehe za
kumuenzi na kumbukumbu ya Baba wa Taifa miaka 20 baada ya kifo chake.
Kwa
mujibu wa Butiku wakati wa ufunguzi wa jengo hilo pia kutafanyika
Kongamano la Kimataifa kuhusu kazi za Taasisi ya Mwalimu ikuhusisha
Amani,Umoja na Maendeleo yenye tija kwa watu wote huku msisitizo ukiwa
katika utekelezaji wa sera ya kwenda katika nchi yetu.
Kupitia
kikao hicho, Butiku alipata ushauri kuhusu maeneo ambayo Taasisi ya
Mwalimu Nyerere ingependa hasa maeneo yanayohusu wananchi moja kwa moja
vijijini na mijini na ambayo ni muhimu kwa amani umoja na maendeleo yao
na Taifa kwa ujumla.
Kwa
upande wake Waziri Lukuvi alimshukuru Butiku kwa kumtembelea kwa lengo
la kupata ushauri hasa katika masuala yanayohusu wananchi na kueleza
kuwa kikao chao mbali na kubadilishana uzoefu lakini pia kililenga katika kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo huku msisitizo ukiwa ni kuleta Amani na Umoja kwa taifa kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment