Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani
Jafo akifungua semina ya kuandaa maandiko ya miradi ya kimkakatiWashiriki wakimskiliza Waziri Jafo wakati wa ufunguzi semina ya kuandaa maandiko ya miradi ya kimkakatiMkurugenzi
Msaidizi Idara ya Serikali za Mitaa Angelista Kihaga atoa neno la
utangulizi wakati wa ufunguzi wa semina ya kuandaa maandiko ya miradi ya
kimakatiWaziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
…………………
Nteghenjwa Hosseah,OR-TAMISEMI
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo ameionya mikoa ya
Dodoma,Lindi na Njombe iliyoshindwa kupeleka watendaji wake kuhuduhuria
semina ya kuandika miradi ya kimkakati.
Onyo hilo juzi jijini hapa wakati
akifungua semina ya siku mbili iliyoshirikisha mamlaka za serikali za
mitaa zilizopo Tanzania Bara na sekretarieti za mikoa semina
iliyofanyika katika Chuo cha serikali za mitaa Hombolo.
Jafo alisema semina hiyo ni muhimu sana
kwao kwa ajili ya kuwajengea uwezo utakaowawezesha kuibua miradi
mbalimbali lakini ameshangaa mikoa hiyo kutopeleka watendaji wake.
“Hapa hatuna wawakilishi wa mkoa wa
Dodoma,Njombe na Lindi wakati Dodoma mradi mkakati walioupata ni Kondoa
peke yake,hakuna Bahi,Chamwino wala Jiji,Njombe nao hakuna mradi mkakati
walioupata cha kushangaza kwenye semina hii hawapo,”alisema.
Alieleza Lindi wana mradi mkakati katika
halmashauri ya Liwale na Ruangwa lakini bado hawajahudhuria semina hiyo
na Mtwara halmashauri wana mradi katika halmashauri moja lakini
Nanyumbu,Masasi,Newala,Tandahimba na Nanyamba hakuna mradi wowote
walioupata lakini pia hawajahudhuria.
“Hii Nanyamba ni halmashauri ya mwisho
katika ukusanyaji wa mapato nawaagiza wahakikishe awamu ya pili ya
semina hiyo wanakuwepo,”alisema.
Jafo alisema mpaka sasa kiasi cha
Sh.Bilioni 268.37 zimeshatolewa na serikali kwa ajili ya kugharamia
miradi 38 na hapo kuna halmashauri hazijaguswa na miradi hiyo kutokana
na maandiko yao kutokuwa na sifa za kuweza kupata fedha na hali yao ya
uchumi bado ipo mbaya sana.
“Leo hii unapoona halmashauri zimepewa
nafasi hiyo lakini still zimelala kuanzia wilayani hadi mkoani hapo kuna
matatizo,”alisema Waziri Jafo.
Alibainisha kuwa ni lazima kubadili mbinu
za ukusanyaji wa mapato kwa kuwa serikali lengo lake kubwa ni
kuhakikisha inaondoa mzigo kwa watu wanyonge na ili hizo kodi na tozo
zenye kero ziweze kuondoka ni lazima halmashauri iweze kupata mapato kwa
njia nyingine mbadala.
“Jiji la Dodoma hawapo hapa,sijui kiburi
cha kukusanya mapato mengi ndio maana hawataki kuja hapa na fedha hizo
ujue ni fedha za kwetu tumeandikia miradi sisi ya TSP wala hawajaandika
ya kwao,nilitamani waje hapa wajifunze, leo hii Dodoma mpaka mwezi huu
wameshakusanya Sh.Bilioni 60 wangekuja hapa wangepata maarifa mengine
zaidi,”alisema.
Alizitaka halmashauri kutekeleza miradi
inayopelekwa kwao bila ya kusua sua kwa kuingiza maslahi yao hasa katika
ajenda ya manunuzi ambapo kila mtu anaenda na makaratasi yake ikiwa na
mkadarasi wake hali inayofanya miradi hiyo kutoendelea mbele .
Awali, Mkurugenzi Msaidizi Idara za
Serikali za Mitaa, Angelista Kihaga alisema miradi ya kimkakati ni
utaratibu mpya wa serikali wa kutoa fedha za maendeleo kwa mamlaka za
serikali za mitaa.
Naye, Kaimu Mkuu wa Chuo cha Hombolo Dk.
Michael Msendekwa alisema mafunzo hayo yametokana na tafiti zilizofanywa
na chuo hicho kuonyesha kuna changamoto katika maandishi ya miradi
katika mamlaka za serikali za mitaa.
Alisema mafunzo hayo yanatolewa kwa
ushirikiano baina ya TAMISEMI na Wizara ya Fedha lengo likiwa ni
kuelekezana na kusaidiana kutatua changamoto hiyo.
0 comments:
Post a Comment