Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya
Michezo Nchini, Addo Komba,akisalimiana na viongozi kabla ya uzinduzi
rasmi wa mashindano ya Mpira wa Miguu na Mpira wa Pete ya Buchimwe Cup
2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Buigiri (CCM) Mhe.Kenneth Yindi
wilaya ya Chamwino.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya
Michezo Nchini, Addo Komba,akitetea jambo na Diwani wa kata ya Buigiri
Mhe.Kenneth Yindi wakati wa uzinduzi rasmi wa mashindano ya Mpira wa
Miguu na Mpira wa Pete ya Buchimwe Cup 2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa
Kata ya Buigiri (CCM) wilaya ya Chamwino.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya
Michezo Nchini, Addo Komba,akisalimiana na Afisa Elimu Kata ya
Buigiri,Emmanuel Lotto baada ya kusoma risala fupi kabla ya uzinduzi
rasmi wa mashindano ya Mpira wa Miguu na Mpira wa Pete ya Buchimwe Cup
2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Buigiri (CCM) (CCM) Mhe.Kenneth
Yindi wilaya ya Chamwino.
Timu ya Buigiri Misheni wakiwa katika pozi la picha kabla ya kumenyana na Uguzi katika mashindano ya Buchimwe Cup 2019.
Kikosi cha timu ya Uguzi wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mpambano wao dhidi ya Buigiri Misheni Buchimwe Cup 2019.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya
Michezo Nchini, Addo Komba akiwa katika picha ya pamoja na waamuzi kabla
ya kuzindua rasmi mashindano ya Mpira wa Miguu na Mpira wa Pete ya
Buchimwe Cup 2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Buigiri (CCM)
wilaya ya Chamwino.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya
Michezo Nchini, Addo Komba akiwa katika picha ya pamoja na Kikosi cha
timu ya Uguzi FC kabla ya kuzindua rasmi mashindano ya Mpira wa Miguu
na Mpira wa Pete ya Buchimwe Cup 2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa Kata
ya Buigiri (CCM) wilaya ya Chamwino.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya
Michezo Nchini, Addo Komba akiwa katika picha ya pamoja na Kikosi cha
timu ya Buigiri Misheni FC kabla ya kuzindua rasmi mashindano ya
Mpira wa Miguu na Mpira wa Pete ya Buchimwe Cup 2019 yaliyoandaliwa na
Diwani wa Kata ya Buigiri (CCM) wilaya ya Chamwino.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya
Michezo Nchini, Addo Komba akiwa katika picha ya pamoja na Kikundi cha
ngoma kabla ya kuzindua rasmi mashindano ya Mpira wa Miguu na Mpira wa
Pete ya Buchimwe Cup 2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Buigiri
(CCM) wilaya ya Chamwino.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya
Michezo Nchini, Addo Komba akizungumza na timu zote za Buigiri Misheni
na Uguzi FC akiwa kabla ya kuzindua rasmi mashindano ya Mpira wa Miguu
na Mpira wa Pete ya Buchimwe Cup 2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa Kata
ya Buigiri (CCM) wilaya ya Chamwino.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya
Michezo Nchini, Addo Komba akipiga penalti kuashiria uzinduzi mashindano
ya Mpira wa Miguu na Mpira wa Pete ya Buchimwe Cup 2019 yaliyoandaliwa
na Diwani wa Kata ya Buigiri (CCM) wilaya ya Chamwino.
Wachezaji wakitivuana katika mpambano mkali kati ya Buigiri Misheni na Uguzi FC timu hizo zilitoka sare ya kufungana goli 1-1.
Diwani wa Kata ya Buigiri Mhe Yindi
akitoa zawadi ya shilingi elfu tano kwa mchezaji bora wa mechi kutoka
timu ya Buigiri Misheni katika mashindano ya Buchimwe Cup 2019.Picha na
Alex Mathias
…………………..
Na.Alex Mathias,Buigiri,Dodoma
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya
Michezo Nchini, Addo Komba amezindua rasmi mashindano ya Mpira wa Miguu
na Mpira wa Pete ya Buchimwe Cup 2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa Kata
ya Buigiri (CCM) wilaya ya Chamwino.
Mashindano hayo yanashirikisha Timu nane
Kwa kila mchezo ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia Kombe, Seti Moja
ya Jezi na kiasi cha Sh 100,000 taslimu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo Komba
amesema Serikali kupitia Wizara ya Michezo itaendelea kuunga mkono
maendeleo ya Michezo kwani wanaamini licha ya Michezo kuwa ni Afya
lakini siku hizi imekua ni Ajira ambayo imenufaisha kundi kubwa la
vijana.
” Nimpongeze Diwani wenu, Mhe Yindi kwa
kuandaa mashindano haya, kila mwaka amekua akianzisha Ligi mbalimbali
kwa ajili yenu, hii ni faida kwenu na myatumie mashindano haya kukuza
vipaji venu na kuhakikisha mnapiga hatua nyingine ya kupata Timu
zinashoriki Ligi kubwa,” amesema Komba.
Nae Diwani wa Kata hiyo Mhe Yindi amesema
pamoja na kuanzisha mashindano hayo pia kutakua na kozi za uamuzi kwa
vijana waliomaliza kidato cha nne ambazo zitaendeshwa na wakufunzi
kutoka Chama Cha Soka Mkoa wa Dodoma, (DOREFA).
” Lengo la mashindano haya ni kuhakikisha
vijana wetu wanapiga hatua, lakini pia kuunga mkono juhudi za Mhe Rais
Dk John Magufuli kukuza sekta ya Michezo nchini, na sisi kama watu
tunaomsaidia inatubidi kumuunga mkono kwa vitendo.
” Tunafahamu kuwa mna changamoto ya
viwanja vya kuchezea, nimeshaanza kushughulikia na nina hakika kupitia
Wizara ya Michezo tutamaliza changamoto hiyo,” amesema Mhe Yindi.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la
Chinonwa, Mhe Joel Mwaka amempongeza Diwani Yindi kwa kuandaa mashindano
hayo na kuahidi kutoa mchango wake wa hali na mali katika kila hatua ya
mashindano hayo.
Nao wananchi wa Kata hiyo wamemshukuru
Diwani huyo kwa kudhamini upatikanaji wa Jezi na Mipira kwa kila timu
zinazoshiriki Ligi hiyo kwani kumeongeza ari ya kufanya vema.
0 comments:
Post a Comment