Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini
kitabu cha maombolezo ya kifo cha Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki la
Mtwara, Mhashamu Gabriel Mmole katika mazishi yaliyofanyika kwenye
Kanisa Kuu la Watakatifu Wote Mjini Mtwara, Mei 21, 2019. Kulia ni
Askofu wa Jimbo la Geita na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu
Katoliki Tanzania (TEC), Flavian Kasalla.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais
Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mheshimiwa Benjamin Mkapa wakishiriki katika
Ibada ya mazishi ya Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoloki la Mtwara,
Mhashamu, Gabriel Mmole iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo la Mtwara,Titus
Mdoe (kushoto) kwenye Kanisa Kuu la Watakatifu Wote mjini Mtwara, Mei
21, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka
udongo kwenye kaburi la Askofu Mstaafu wa Jimbo la Mtwara, Mhashamu
Gebriel Mmole katika mazishi yaliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la
Watakatifu Wote mjini Mtwara, Mei 21, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka
shada la maua kwenye kaburi la Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki la
Mtwara, Mhashamu, Gabriel Mmole katika mazishi yaliyofanyika kwenye
Kanisa la Watakatifu Wote mjini Mtwara, Mei 21, 2019
Waombolezaji wakiuweka kaburini mwili wa
Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki la Mtwara, Mhashamu Gabriel Mmole
katika mazishi yaliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Watakatifu Wote mjini
Mtwara, Mei 21, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole
Askofu wa Jimbo Katoliki la Mtwara, Titus Joseph Mdoe katika mazishi ya
Askofu Mstaafu wa Jimbo Katolki la Mtwara, Mhashamu Gabriel Mmole
yaliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Watakatifu Wote mjini Mtwara, Mei 21,
2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza
katika Mazishi ya Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki la Mtwara,Mhashamu
Gebriel Mmole kwenye Kanisa Kuu la Watakatifu Wote mjini Mtwara, Mei 21,
2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito
kwa Watanzania wote wamuenzi marehemu Askofu Mstaafu Gaberiel Mmole (80)
wa Jimbo Katoliki Mtwara kwa wema, upole na utumishi mwema aliouonesha
wakati wote wa maisha yake.
Ametoa wito huo leo (Jumanne, Mei 21,
2019) wakati wa mazishi ya Askofu Mmole yaliyofanyika katika Kanisa
Katoliki Mtwara na kuhudhuriwa na viongozi, waumini wa Kanisa Katoliki
pamoja na wakazi wa mkoa wa Mtwara
Askofu Mmole alizaliwa Januari Mosi, 1939
katika Parokia ya Nangoo, ambapo alibatizwa na kupata kipaimara Oktoba
5, 1952. Mwaka 1971 alipata daraja ya upadre na kuwa Askofu kuanzia
mwaka 1988, alifariki Mei 15, 2019 Mkoani Mtwara baada ya kuugua kwa
muda mrefu.
Maeneo aliyoyatumikia tangu apate daraja
la padri ni Paroko msaidizi wa Mnero (1972), Pastoral Institute
GABA-Uganda (1973), Gombera Namupa seminari (1974 hadi Mei 1988),
alitangazwa kuwa askofu wa Jimbo la Mtwara Machi 12, 1988 na alisimikwa
kuwa askofu wa Jimbo la Mtwara Mei 25, 1988.
Mwaka 1951 hadi 1954 alipata elimu ya
singi katika shule ya msingi Ndanda, 1955 alisoma Nyangao Middle School,
1956 akahamia Lukuledi ambako alihitimu 1958. Alienda chuo cha ualimu
Peramiho 1959 hadi 1960, ambapo 1962 alijiunga na seminari ndogo ya
Namupa na alihitimu 1964.
1965 hadi 1966 alichukua masomo ya
falsafa kwenye seminari kuu ya Peramiho na mwaka 1967 hadi 1971
alichukua masomo ya theolojia katika seminari hiyo hiyo ya Peramiho.
1971 alifanya mitihani ya Baccalaureate inayotoka chuo kikuu cha Kipapa
Urbaniana Roma na kupata shahada ya theolojia.
Ibada ya mazishi imeongozwa na Askofu
Mkuu wa Jimbo la Songea, Mhashamu Askofu Damian Dallu ambaye alitumia
muda huo kuwaasa Watanzania kuishi katika maadili mema na kuheshimiana.
Waziri Mkuu amesema enzi za uhai wake
Askofu Mmole alitoa kipaumbele katika masuala muhimu ya maendeleo ya
jamii ikiwemo elimu ambapo alisaidia sana watawa waliomaliza darasa la
saba na kuwasaidia wajiunge na shule za sekondari.
“Hata uanzishwaji wa chuo kikuu cha
STEMMUCO ambacho ni tawi la SAUT hapa Mtwara ni moja ya jitihada zake
alizozifanya katika kuhakikisha anawapa elimu bora vijana na jamii.
Kifo chake ni pigo kubwa kwa Taifa kwa
sababu tumepoteza kiongozi wa kiroho aliyesimamia kwa uadilifu ustawi wa
jamii ya Kitanzania.”
Kwa upande wake, Rais wa
Baraza la Maaskofu Tanzania, Mhashamu Askofu Gervas Nyaisonga wa Jimbo
Kuu la Mbeya amesema wamepata simanzi kubwa kufuatia kifo cha Askofu
Mmole kwani walitegemea hekima zake katika Baraza la Maaskofu.
Ameongeza kuwa Askofu Mmole alikuwa
kielelezo cha dhamira njema na alilitumikia kanisa katika hali yoyote,
hivyo yatupasa kumuombea apumzike kwa amani.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa
Mtwara, Gelasius Byakanwaaliwashukuru viongozi wa madhehebu mbalimbali
ya dini mkoani Mtwara kutokana kwa ushirikiano mzuri anaopata
unaomwezesha kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Mazishi hayo yamehudhuriwa na maelfu ya
wananchi, maaskofu wa majimbo mbalimbali nchini, Rais Mstaafu wa awamu
ya tatu, Mheshimiwa Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa, Waziri wa
Nchi OR-Utumishi na Utawala Bora Mheshimiwa Huruma George Mkuchika.
0 comments:
Post a Comment