Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari
–MAELEZO anayeshughulikia Habari na Picha, Rodney Thadeus akizungumza na
Waaandishi wa Habari wa Redio za Kijamii walipotembelea kujifunza
shughuli za Idara ya Habari leo Jijini Dodoma. Waandishi hao wapo jijini
Dodoma kwa ajili ya mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wa
utendaji kazi wao. Kutoka kulia ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo ambaye pia
ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine (SAUT), Dotto Bulendu
na Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO, Abuu Kimario.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Habari
Tanzania (TADIO), Prosper Kwigize akielezea jambo wakati wa ziara ya
Waandishi wa Habari wa Radio za Kijamii katika Ofisi za Idara ya Habari –
MAELEZO kwa ajili ya kujifunza shughuli za Idara hiyo leo Jijini
Dodoma. Waandishi hao wapo jijini Dodoma kwa ajili ya mafunzo ya siku
mbili ya kuwajengea uwezo wa utendaji kazi wao. Kutoka kulia ni Mkufunzi
wa Mafunzo hayo ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu
Agustine (SAUT), Dotto Bulendu, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari
–MAELEZO anayeshughulikia Habari na Picha, Rodney Thadeus na Afisa
Habari wa Idara ya Habari MAELEZO, Abuu Kimario.
Afisa Habari wa Idara ya Habari – MAELEZO,
Bi. Beatrice Lyimo akifafanua kuhusu taratibu za namna ya kupata
Vitambulisho vya Waandishi wa Habari “Press Card” wakati ziara ya
Waandishi wa Habari wa Radio za Kijamii kwa lengo la kujifunza shughuli
za Idara hiyo leo jijini Dodoma.
Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Radio ya
Kijamii Sibuka FM kilichopo Maswa Mkoani Simiyu, Nicholaus Machunda
akionyesha Kitambulisho cha Uandishi wa Habari “Press Card” mara baada
ya kukamilisha taratibu na kukabidhi wakati wa ziara ya Waandishi wa
Habari wa Radio za Kijamii katika Ofisi ya Idara ya Habari – MAELEZO leo
Jijini Dodoma. Waandishi hao wapo jijini Dodoma kwa ajili ya mafunzo ya
siku mbili ya kuwajengea uwezo wa utendaji kazi wao.
Baadhi ya Waandishi wa Habari toka Radio za
Kijamii wakifuatilia maelezo ya Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari
–MAELEZO anayeshughulikia Habari na Picha, Rodney Thadeus wakati wa
ziara yao ya kujifunza namna Idara ya Habari – MAELEZO inavyofanya kazi
leo Jijini Dodoma. Waandishi hao wapo jijini Dodoma kwa ajili ya mafunzo
ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wa utendaji kazi wao.
Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Radio ya
Kijamii Pambazuko FM ya Ifakara Morogoro, Amina Mrisho akichangia mada
wakati wa ziara ya Waandishi wa Habari wa Radio za Kijamii katika Ofisi
ya Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dodoma. Waandishi hao wapo
jijini Dodoma kwa ajili ya mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wa
utendaji kazi wao.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari
–MAELEZO anayeshughulikia Habari na Picha, Rodney Thadeus (kushoto)
akiagana na Mkufunzi wa Mafunzo hayo ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo
Kikuu cha Mtakatifu Agustine (SAUT), Dotto Bulendu mara baada ya
kumaliza mazungumzo na Waaandishi wa Habari za Radio za Kijamii
walipotembelea Idara hiyo kwa lengo la kujifunza leo Jijini Dodoma.
Waandishi hao wapo jijini Dodoma kwa ajili ya mafunzo ya siku mbili ya
kuwajengea uwezo wa utendaji kazi wao.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari
–MAELEZO anayeshughulikia Habari na Picha, Rodney Thadeus (kulia)
akiagana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Habari Tanzania
(TADIO), Prosper Kwigize mara baada ya kumaliza mazungumzo na Waaandishi
wa Habari za Radio za Kijamii walipotembelea Idara hiyo kwa lengo la
kujifunza leo Jijini Dodoma. Waandishi hao wapo jijini Dodoma kwa ajili
ya mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wa utendaji kazi wao.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO anayeshughulikia Habari na Picha,
Rodney Thadeus (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waaandishi wa
Habari za Radio za Kijamii walipotembelea Idara ya Habari –MAELEZO kwa
lengo la kujifunza leo Jijini Dodoma. Waandishi hao wapo jijini Dodoma
kwa ajili ya mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wa utendaji kazi
wao. (Picha na Frank Shija)
0 comments:
Post a Comment