Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa Masheikh wa
Mikoa ya Kanda ya Kati, Wazee wa Dodoma, Wabunge, Viongozi wa Dini,
Wananchi, wawakilishi wa Taasisi mbalimbali na wafanyakazi wa NMB kwenye
hoteli ya Dodoma, Mei 24, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa Masheikh wa
Mikoa ya Kanda ya Kati, Wazee wa Dodoma, Wabunge, Viongozi wa Dini,
Wananchi, wawakilishi wa Taasisi mbalimbali na wafanyakazi wa NMB kwenye
hoteli ya Dodoma, Mei 24, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Albert Jonkergouw
katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa Masheikh wa Mikoa ya
Kanda ya Kati, Wazee wa Dodoma, Wabunge, Viongozi wa Dini, Wananchi,
wawakilishi wa Taasisi mbalimbali na wafanyakazi wa NMB kwenye hoteli ya
Dodoma, Mei 24, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katika
futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa Masheikh wa Mikoa ya Kanda
ya Kati, Wazee wa Dodoma, Wabunge, Viongozi wa Dini, Wananchi,
wawakilishi wa Taasisi mbalimbali na wafanyakazi wa NMB kwenye hoteli ya
Dodoma, Mei 24, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewataka Watanzania watumie Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kudumisha
amani na mshikamano na kuwaombea viongozi wa kitaifa.
“Mwezi huu tuna majukumu makubwa
ya kufanya ibada, kutubu dhambi zetu na kuomba rehma kwa Mwenyezi Mungu
pamoja na kudumisha mshikamano na kuwa wavumilivu.”
Waziri Mkuu alitoa wito huo jana
jioni (Ijumaa, Mei 24, 2019) aliposhiriki hafla ya futari iliyoandaliwa
na benki ya NMB iliyofanyika katika Hoteli ya Dodoma.
Alisema kila wananchi aendelee
kuliombea Taifa lizidi kudumisha amani na mshikamano. “Tuhakikishe
tunatenda matendo mema yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu.”
Kadhalika, Waziri Mkuu alitumia
fursa hiyo kuipongeza benki ya NMB kwa huduma bora wanazozitoa kwa
wananchi ikiwa ni pamoja na kuwa na matawi mengi hadi vijijini.
Awali, Mkurugenzi wa benki ya
NMB, Albert Jonkergouwalisema lengo la kuandaa hafla hiyo ya futari ni
kuimarisha ushirikiano uliopo baina yao na wateja wao.
Mkurugenzi huyo alisema katika
kipindi hiki Waislamu wanapaswa kumrudia Muumba wao na kumshukuru kwa
mema yote anayowajalia waja wake.
“Mwezi wa Ramadhan ni kipindi
muafaka cha kufuturu pamoja hivyo, nawashukuru wateja wetu kwa kujumuika
nasi nawaomba muendelee kutumia huduma zetu.”
Alisema mkusanyiko huo
unadhihirisha kuwa wao ni sehemu ya jamii ya Watanzania wote, hivyo
aliwasisitiza wateja wa benki hiyo waendelee kutumia zaidi huduma za
kidijitali.
Hafla hiyo ilihudhuliwa na Spika
wa Bunge, Job Ndugai, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Mashekhe wa Mikoa
ya Kanda ya Kati (Dodoma, Singida na Manyara).
Wengine ni Wazee wa Dodoma,
Waheshimiwa Wabunge , Viongozi wa dini, wananchi, Wawakilishi wa Taasisi
mbalimbali na Wafanyakazi wa NMB.
0 comments:
Post a Comment