METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, May 28, 2019

STAND UNITED ‘CHAMA LA WANA’ YAIFUATA AFRICAN LYON LIGI DARAJA LA KWANZA

Na Mwandishi Wetu.
TIMU ya Stand United ya Shinyanga, maarufu kama Chama la Wana’ leo imeipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuchapwa mabao 2-0 na JKT Tanzania 2-0 Uwanja wa Meja Isamuhyo, Mbweni mjini Dar es Salaam.
Mabao yaliyoizamisha Stand United leo yamefungwa na washambuliaji wa JKT Tanzania, Samuel  Kamuntu dakika ya 51 na Najim Magulu dakika ya 73.
JKT Tanzania iliyorejea msimu huu Ligi Kuu, imenusurika kushuka baada ya kumaliza na pointi 47 katika nafasi ya 10, wakati Stand United imemaliza nafasi ya 19 kwa pointi zake 44, ikiungana na African Lyon kuteremka daraja.
Nazo Kagera Sugar ya Bukoba na Mwadui FC ya Shinyanga zitamenyana na timu za Daraja la Kwanza, Pamba SC na geita Gold kuwania kubaki Ligi Kuu katika mechi za mchujo.
Hiyo ni baada ya Kagera Sugar inayofundishwa na Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Mecky Mexime kulazimishwa sare ya 1-1 na Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza na Stand United kushinda 3-1 dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Kagera Sugar imemaliza nafasi ya 18 kwa pointi zake 44 sawa na Mwadui iliyomaliza ya 17 kwa wastani nafuu wa mabao.

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA LIGI KUU LEO
Coastal Union 0-0 Singida United.
Mbeya City 0-0 Biashara United.
Mtibwa Sugar 0-0 Simba SC.
Ruvu Shooting 1-0 Alliance FC (Fully Zullu Maganga 25’ p) . .
JKT Tanzania 2-0 Stand United (Samweli Kamuntu 51’, Najimu Maguli 73’).
Ndanda SC 1-3 Mwadui FC (Kigi Makasi : Ottu Joseph 39’, 41’, Salim Aiyee 61’) .
Yanga SC 0-2 Azam FC (Daniel Amoah 45’+2, Mudathir Yahya 50’).
Mbao FC 1-1 Kagera Sugar (Hebert Lukindo 60’ : Ally Ramadhan 20’).
Tanzania Prisons 3-1 Lipuli FC (Benjamini Asukile 29’, Adam Adam 48’, 85’ : Seif Rashid 46’).
African Lyon 0-2 KMC FC (Cliff Buyoya 21’, 17’)

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com