Na Mwandishi wetu
VINARA wa soka katika michuano ya
Ligi Kuu ya Hispania, LaLiga, timu ya Sevilla FC inatarajiwa kuwasili
nchini kesho kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Simba ikiwa ni
mara ya kwanza katika historia ya kwa timu hiyo kucheza nchini
Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
jana jijini Dar es Salaam, timu hiyo inatarajiwa kuwasili kesho jioni
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Kulingana na taarifa hiyo mechi
hiyo itakuwa ni maalum kwa vinara hao wa ‘LaLiga ambao wanadhaminiwa na
SportPesa’ na akaongeza kwamba ziara itahusisha matukio kadhaa ya
jamii na michezo ikiwemo kliniki namafunzo mbalimbali.
“Kama ushindani wa kimataifa unakutana na dhamira ya LaLiga kuwa karibu na mashabiki wake.
Kwa kweli kwamba mashabiki wetu
wa Tanzania wataweza kupata furasa ya kuangalia karibu klabu kubwa
kama Sevilla FC inamaanisha kuwa ni fursa kubwa kwa kila mtu,” alisema
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Kimataifa katika Ligi ya La Liga, Oscar Mayo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
Usimamizi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Tarimba Abbas, kampuni
yao imeshirikiana na baadhi ya taasisi za soka za kubwa ulimwenguni
baada ya kuna kuna haja ya kuleta uzoefu huu mkubwa kwa Tanzania.
“Ili kufurahia kuona moja ya
klabu kubwa za mpira wa miguu Ulaya, Sevilla FC. Kwa makubaliano yetu
na LaLiga ambayo ni ligi bora duniani, tutaweza kuonyesha vipaji vyetu
na kuboresha kiwango cha soka nchini “, alisema Talimba.
Alisema kwamba mechi hiyo ni
sehemu ya mradi wa ‘LaLiga duniani ambao unalenga kueneza soka la
Hispania kimataifa na kueneza pia sera ya ‘Marca España’, kuleta
karibu mashabiki wa LaLiga na kukuza klabu nje ya nchi yetu.
Hii itakuwa ni klabu ya pili
Ulaya kufanya ziara Afrika Mashariki, baada ya mwaka 2017 Everton FC
kucheza na Gor Mahia nchini Kenya, ingawa sio mara ya kwanza kwa
Sevilla kutua katika bara hili kwani mwaka 2015 ilikuwa nchini
Morocco ambao ilicheza mechi ya kuajindaa na LaLiga dhidi ya timu ya
Hassania Union Sport d’Agadir.
0 comments:
Post a Comment