Mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) manispaa ya Iringa, Ashura Jongo akiongea na mwandishi wa habari wa blog hii katika mahojiano maalum yaliyofanyika katika viwanja halmashauri ya manispaa ya Iringa kuhusu wanawake wanaweza kuwa viongozi wazuri tatizo ni kushindwa kuthubutu
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) manispaa ya Iringa, Ashura Jongo akiwa tayari kwa ajili ya mahojiano na mwandishi wa blog hii
NA
FREDY MGUNDA,IRINGA.
WANAWAKE
manispaa ya Iringa wametakiwa kushiriki katika chaguzi mbalimbali
zinazojitokeza hapa nchini ili kuongoza jamii inayowazunguka.
Akizungumza
na blog hii mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT)
manispaa ya Iringa, Ashura Jongo alisema kuwa wanawake wanaweza kuwa viongozi
wazuri tatizo ni kushindwa kuthubutu.
“Tangu
mkutano wa beijing china umefanikisha kutujengea uwezo wananwake kwa kupata
semina mbalimbali ambazo zimetusaidia kuwa viongozi wazuri wa kuweza kuongoza
kwenye kila idara hivyo mkutano ule ulitusaidia sana wanawake” alisema Jongo
Jongo
alisema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikiwathamini
wanawake kwa kuwapatia nafasi mbalimba za uongozi ambazo pia wanawake hao
wamekuwa wakizitendea haki nafasi hizo.
“Nyinyi
wenyewe mmekuwa mashaidi kuwa marais wetu wa awamu ya nne na serikali ya awamu
ya tano mmeona jinsi gani viongozi wanawake wameongezaka katika nafasi
mbalimbali za uongozi hasa kwenye nafasi za kuteuliwa na kuchaguliwa” alisema Jongo
Alisema
kuwa ilikuwa vigumu mno kuona Rais akichagua viongozi wengi wanawake kama
ilivyo hivi sasa ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe
Magufuli ameua mawaziri wengi wanawake,wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa pamoja na
wakurugenzi kutoka sekta mbalimbali kwenye serikali ya awamu ya tano.
“Mmekuwa
mashahidi mkiwaona viongozi wanawake walioteuliwa na waliogombea jinsi gani
wanafanya kazi sawa sawa na wanaume hivyo wanawake tutaendelea kujiamini na
kuongoza vizuri kati ngazi mbalimbali ambazo tutapata nafasi ya kuongoza”
alisema Jongo
Aidha
Jongo aliwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi kwa
kuwa wanawake wamekuwa viongozi wazuri ila tatizo ni kushindwa kuthubutu.
“Saizi
wanawake hawatakiwi kuwa na uoga wa kugombea mnatakiwa kukimbilia nafasi yeyote
ili inayojitokeza kugombea kwa kuwa mnauwezo wa kuongoza na mmeonyesha kuwa
mnaweza” alisema Jongo
Lakini
Jongo aliwataka wanaume kuwapa nafasi wanawake kugombea nafasi mbalimbali na
kuwaondolea uoga kwa kuwa wanaweza kuongoza katika nafasi nyeti za serikali.
Jongo alimalizia kwa kusema kuwa wanawake wamekuwa
viongozi hata kwenye familia ndio maana familia nyingi ambazo wanawake wamepewa
nafasi wamekuwa viongozi wazuri wa familia.
0 comments:
Post a Comment