Na. OWM, MOROGORO
Mtandao wa Afya moja kwa nchi za
Afrika mashariki, Kati na Magharibi (OHCEA) umeendesha mafunzo ya Dhana ya Afya
moja kwa wanafunzi wa ngazi ya Stashahada na Astashahada kutoka vyuo vya
kwenye sekta za Afya ya Binadamu, Mifungo, Wanyamapori na Mazingira. Tanzania
imekuwa nchi ya kwanza Duniani kufundisha Dhana hiyo katika ngazi hizo za
taaluma, kwa kuwa nchi nyingine duniani hufundisha tu kwa ngazi ya
Shahada na Shahada ya Uzamivu masuala ya Afya moja.
Dhana ya Afya moja ambayo ni
ushirikishwaji wa pamoja sekta ya Afya ya Binadamu, Wanyamapori, Mfugo,
Kilimo na mazingira katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili
magonjwa yatokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu ama kinyume chake. Wataalamu
hao wamepata mafunzo hayo kwakuwa wapo karibu sana na jamii na pindi
utokeapo mlipuko wa ugonjwa ndio huwa kikosi kazi cha kwanza na mstari wa
mbele kuwa eneo la tukio katika kufuatilia na kukabili milipuko,
kabla ya wataalamu wengine kushiriki kikamilifu.
Akiongea wakati wa kufunga Warsha ya kufanya tathmini ya namna wakufunzi wanavyotumia
mitaala ya Afya Moja katika kuwafundisha wanafunzi wao wa ngazi ya Stashahada
na Astashahada, tarehe 13 Aprili, Mjini Morogoro, Mkurugenzi wa Idara ya
Uratibu wa Shughuli za Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe
alifafanua kuwa mafunzo hayo yanajenga kikosi kazi imara chenye kuchagiza
shughuli za Afya moja hapa nchini.
“Katika kuimarisha Afya ya Binadamu pamoja na
Afya ya mifugo na wanyamapori, kwa kutumia Dhana ya Afya moja, ninafarijika kwa
jitihada hizi za kuwajengea uwezo Wataalamu wa sekta za Afya katika ngazi
ya Stashahada na Astashahada pamoja na wakufunzi wao, kwa kuwa tunaandaa rasilimali
watu ya kuweza kuwa na uwezo wa kujiandaa, kufuatilia na kukabili
magonjwa kwa Dhana ya Afya moja. Alisema Matamwe.
Wakiongea kwa nyakati tofauti waratibu wa
mafunzo hayo Profesa; Japheti Killewo na Profesa. Robinson Mdegela
walifafanua kuwa tayari mitaala ya Afya moja kwa ngazi ya stashahada na
astashahada imekamilika, lakini wakati taratibu za kuingiza masuala ya
Afya moja zitakamilika hivi karibuni katika mitaala ya ngazi ya
stashahada na Astashahada wameamua kufanya mafunzo hayo ili wakufunzi kujifunza
kwa vitendo juu ya kufundisha masuala ya Afya moja lakini pia na kuwaandaa
wanafunzi watakao fundishwa kwa kutumia mitaala hiyo.
Aidha waratibu hao walibainisha kuwa wanafunzi hao wakiweza kuielewa vizuri dhana ya
Afya moja watatumika vyema kuielimisha jamii juu ya masuala ya Afya Moja,
na nchi yetu itaweza kuzuia maambukizi ya magonjwa ya mlipuko hususani
yale yatokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu na pia kupunguza usugu wa madawa
kwa sababu wataweza kuongeza ushirikiano, mawasiliano na uratibu baina ya sekta
husika.
Mafunzo hayo
yaliyowajumuisha zaidi ya wanafunzi 210, wa ngazi ya astashahada na
ngazi ya cheti kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili,
SUA, Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Morogoro, Chuo cha Afya cha Kilosa,
Chuo cha Wanyamapori Pasiansi na Chuo cha Wanyamapori Mweka.
Aidha, wakufunzi zaidi ya 30 wameshiriki kutoka Chuo Chuo
Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Chuo kikuu cha Kilimo Sokoine,
Vyuo vya Afya Lindi, Mafinga, Kilosa, Mtwara, Singida, Kagemu, Mirembe, Wakala
wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Morogoro, Temeke, Tengeru, Buhuri, pamoja na Vyuo
vya Taaluma ya Wanyamapori , Pasiansi na Mweka.
Mafunzo hayo yameratibiwa na Chuo Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili na Chuo kikuu cha Kilimo Sokoine kwa kushirikiana
na USAID, kupitia vyuo vikikuu
vya MINNESOTA na Tufs vya nchini Marekani
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment