Na Mwandishi Wetu
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeungana familia,
ndugu, jamaa na marafiki kuuaga na kuuhifadhi
kwenye makazi yake ya milele, mwili wa
mtumishi wake Clarence Nanyaro aliyefariki Aprili 2 mwaka huu na kuzikwa
kijijini kwao Nkomaala, wilayani Meru mkoani Arusha.
Tume katika mazinshi hayo iliwakilishwa na
Mkurugenzi Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Zanzibar, Felix Wandwe
aliyeambatana na baadhi ya watumishi kumhifahdi marehemu Nanyaro aliyekuwa
Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Habari wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura.
Akizungumza wakati akitoa salamu za
rambirambi, Mkurugenzi Wandwe alisema Tume inaungana na familia, ndugu, jamaa
na marafiki kuombeleza msiba wa mtumishi wake kwani marehemu Nanyaro alikuwa
mtu wa kuaminiwa kutokana na utendaji kazi wake mzuri.
“Kwa niaba
ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi napenda kuwasilisha salamu za rambirambi
kwa masikitiko makubwa.Marehemu alifanya kazi vizuri sana na tulimuamini na
kumpenda, lakini kwa mapenzi ya Mungu
amemchukua, tunasema Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidewe”
alisema Mkurugenzi Wandwe na kuongeza kuwa.
“Kuhusiana na suala la rambirambi napenda
kueleza kwamba Ofisi inafanya utaratibu wa michango mbalimbali ambayo baada ya hapa tutawasiliana na familia kujua
utaratubu wa kuwasilisha.”
“Pili kwa kuwa marehemu alikuwa mtumishi wa
Serikali, kwa niaba ya Tume niseme kwamba zitafanyika taratibu za kisheria, kanuni
na taratibu kuhusiana na stahiki zake na atapewa mtu kama sheria zinavyoelekeza”.
Akitoa shukrani kwa niaba ya familia, Mkuu wa
Boma Mzee Gadiel Nanyaro aliishukuru Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa huduma
waliyoitoa kwa marehemu na kumuomba mwakilishi wake kufikisha shukrani hizo
ofisini kutokana na ushirikiano mkubwa waliyoutoa kwa familia.
Marehemu Nanyaro mbali na kufanya kazi Tume
tangu mwaka 2015 hadi umauti unamkuta, pia alifanya kazi Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Ofisi ya
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Utangazaji
(TBC) kwa nafasi mbalimbali.
Alifariki tarehe 2 Aprili mwaka huu kutokana
na kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na hivi karibuni alipata ‘Mild Stroke’
ambao ulisababisha alazwe kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa takribani
siku 19 hadi umauti ulivyomkuta.
Akisoma akitoa salamu za rambirambi wakati
watumishi wa Tume wakiaga mwili wa marehemu jijini Dar es Salaam, Mkugenzi wa
Habari na Elimu ya Mpiga Kura ya NEC, Giveness Aswile alisema alitoa shukrani za
Tume kwa madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali
ya Bochi kwa jitihada walizofanya katika kuokoa uhai wa marehemu.
“Tume inatoa shukrani kwa madaktari na wauguzi
wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali ya Bochi kwa jitihada
walizofanya katika kuokoa uhai wa marehemu.Pia inawashukuru viongozi wa dini,
watu binafsi na taasisi mbalimbali kwa kumuhudumia marehemu wakati wa uhai
wake.” alisema Mkurugenzi Aswile.
Marehemu ameacha mjane na watoto.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana
lihimidiwe.
0 comments:
Post a Comment