Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa siku tatu kwa wakuu wa
wilaya wanaosimamia halmashauri ambazo Mwenge wa Uhuru umekataa kuweka mawe ya
msingi au kuzindua miradi iliyopitiwa na Mwenge huo kutoa maelezezo ya kina juu
ya sababu ya kukataliwa kwa miradi hiyo yenye tamani ya shilingi 1,248,489,871.
“Napenda nitoe maelekezo kwa Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya wenye miradi
iliyokataliwa kunipa taarifa ya kwanini miradi yao haikuzinduliwa/kuwekewa mawe
ya msingi. Maelezo hayo niyapate ndani ya siku tatu kuanzia tarehe ya leo hadi
tarehe 14, April, 2019,” Alisisitiza.
Ameyasema hayo muda mfupi kabla ya kukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Mh. Amos Makalla huku Mwenge huo ukiwa umekimbizwa katika
halmashauri nne za Mkoa wa Rukwa zikichukua umbali wa kilemeta 832.5 na
kutembelea miradi 35 na vikundi 11 ikiwa na tamani ya shilingi
45,404,104,489.59
Aidha, kutokana na mbio hizo za Mwenge wa Uhuru kubeba kauli mbiu
isemayo “Maji ni haki ya Kila mtu, tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki
uchaguzi wa serikali za mitaa,” hivyo alitoa wito kwa wananachi kuendela
kutunza vyanzo vya maji, kuimarisha jumuia za watumia maji pamoja na kufanya
maandalizi thabiti ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na kujitokeza kwa
wingi katika uchaguzi huo.
Kwa upande wake Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2019 Ndugu Mzee
Mkongea Ali aliushukuru uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa kumpa ushirikiano wa
Kutosha tangu wanawasili katika mkoa huo hadi kuondoka na kuelekea katika mkoa
wa Katavi na kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa kufikisha asilimia 55 ya
wananchi wa Mkoa huo kupata maji safi na salam.
“Mimi nikupe hongera kwasababu takwimu zinaonyesha katika mkoa wako wa
Rukwa umejitahidi kwa asilimia 55 kuhakikisha wananchi woyte wanapata maji ya
uhakika na salama sambamba na hilo katika kupambana na Rushwa katika TAKUKURU
kuna malalamiko 64 na kesi 59 wanazifanyia kazi, endeleeni kufanya kazi na
kuhakikisha haki inapatikana kwa wote,” Alisema.
Kutokana na mapungufu yaliyobainika Mwenge wa Uhuru haukuzindua
amakuweka mawe ya msingi kwenye miradi mitatu, Halmashauri ya Manispaa ya
Sumbawanga mradi mmoja vyumba vitano vya madarasa wenye thamani ya shilingi
76,250,000, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mradi mmoja wa ujenzi wa nyumba
ya waalimu “6 in 1” wenye thamani ya shilingi174,977,775 na Halmashauri ya
Wilaya ya Kalambo mradi mmoja wa maji wenye thamani ya
shilingi 997,262,096.
0 comments:
Post a Comment