Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe (Kushoto) akitazama wakurugenzi wa Bodi zilizopita wakati alipotembelea ofisi za Bodi ya Sukari Jijini Dar es salaam juzi tarehe 9 Aprili 2019. Mwingine pichani ni Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Prof Keneth Benges.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akisalimiana na baadhi ya watendaji wa idara ya uhasibu wakati alipotembelea Bodi ya Sukari
Jijini Dar es salaam juzi tarehe 9 Aprili 2019.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe juzi tarehe 9 Aprili 2019 alifanya ziara ya
kushitukiza kwa kutembelea Bodi ya Sukari Jijini Dar es salaam.
Katika ziara hiyo Mhandisi
Mtigumwe amewasihi wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii, umoja na mshikamano.
Mhandisi Mtigumwe
amewasisitiza wafanyakazi hao kufanya kazi kwa umakini mkubwa na kuhakikisha
kuwa wanaondoa kero zinazowakabili wananchi katika sekta ya sukari.
Katika hatua nyingine Mhandisi
Mtigumwe alipata fursa ya kukagua idara mbalimbali katika ofisi hizo ikiwa ni
pamoja na kupata maelezo kwa kina ya utendaji kazi wake.
0 comments:
Post a Comment