Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akiongea
wakati wa ufunguzi wa mkutano wa
kimataaifa wa nchi wanachama wa Maziwa Makuu kwenye Hotel ya Morena Jijini
Dodo.
Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo
akiongea na wajumbe wa mkutano wa kimataaifa wa nchi wanachama wa Maziwa Makuu
jijini Dodoma.
Na Issa Mtuwa Dodoma
Nchi Wanachama
wa Maziwa Makuu zimetakiwa kushikamana kuunganisha nguvu katika kulinda na kusimamia
matumizi ya rasilimali ardhi ikiwemo madini ili kunufaisha nchi hizo.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Madini Doto Biteko wakati akifungua mkutano wa Kimataifa
wa nchi Wanachama wa Maziwa Makuu (International Conference on the Great Lakes
Region - ICGLR) unaofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 11-12 Machi 2019
katika Hotel ya Morena jijini Dodoma.
Biteko
amezitaka nchi hizo kuunganisha nguvu ya pamoja katika kudhibiti raslimali
ardhi ikiwemo madini na kujiwekea utaratibu utakao dhibiti shughuli za
uzalishaji na biashara ya madini ili raslimali hizo zinufaishe mataifa yao na
zisitumike vibaya.
“Unganisheni
nguvu kwa pamoja, wekeni utaratibu utakao wafanya nchi wanachama kunufaika na
raslimali ardhi/madini. Jitahidini kuhakikisha raslimali hizo hazitumiki vibaya
kama ilivyo kubaliwa kwenye itifaki, hivyo lazima kuwe na utaratibu na sheria
kwa kila nchi namna ya kudhibiti uzalishaji na biashara ya madini,” amesema
Biteko.
Naye,
Mtaalam kutoka Wizara ya Madini, Mhandisi Assah Mwakilembe amesema Mkutano huo
unalenga kujadili na kupitia mfumo wa udhibitisho wa mnyororo wa madini kwa
lengo la kudhibiti uzalishaji na biashara ya madini katika nchi za maziwa makuu
kufuatia kuwepo tetesi zilizo kuwa zinahusisha raslimali ardhi (Madini) na
ufadhili wa vita katika nchi za aaziwa makuu. (Region Certification Manual)
Akizungumza
mara baada ya kuwasilisha mada kuhusu marekebisho ya Sheria Madini ya Mwaka
2017 Mkurugenzi wa Idara ya Sheria kutoka Wizara ya Madini, Edwin Igenge
amesema kwa upande wa Tanzania, imetekeleza itifaki ya pamoja ya nchi wanachama
wa Maziwa Makuu kama ilivyo kubaliwa.
Ameongeza
kuwa, utekelezaji wa itifaki kwa Tanzania ni pamoja na marekebisho ya sheria ya
Madini ya Mwaka 2017 yaliyopelekea kuundwa kwa Tume ya Madini ambapo shuguli
zote za usimamizi wa raslimali madini zimepewa Tume ya Madini ambapo kabla ya
hapo shuguli hizo zilikuwa chini ya Kamishna wa Madini.
Igenge
amesema kuanzishwa kwa itifaki katika nchi za maziwa makuu kulitokana na tetesi
za uwepo wa matumizi mabaya ya raslimali ardhi ikiwemo madini ambapo kipato cha
raslimali hizo inasadikika kuwa zilikuwa zinatumika kufadhili shuguli za za
kivita katika nchi za maziwa makuu, hivyo kupelekea kuanzishwa kwa itifaki ya
pamoja kwa lengo la kudhibiti.
Mkutano
huo wa kimataaifa unahudhuriwa na wajumbe kutoka Tanzania, Burundi, Rwanda na
wawakilishi wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na Sekretariati ya nchi
wanachama wa Maziwa Makuu. Kwa upande wa Tanzania inawakilishwa na Wizara ya Madini,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Shirikisho la
Wachimbaji Tanzania (FEMATA), Chama cha Wanunuzi na Wauzaji wa Madini Tanzania (TAMIDA), Tume ya Madini, Shirika la Madini la
Taifa (STAMICO), Wakala wa Jiolojia na Utafiti
wa Madini (GST).
Katika
mkutano huo, Waziri Biteko aliambatana na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus
Nyongo, Kamishna wa Madini Mhandisi Daivid Mulabwa, Mkurugenzi wa Sheria kutoka
Wizara ya Madini Edwin Igenge na baadhi ya maafisa kutoka wizara ya Madini.
0 comments:
Post a Comment