Waziri
wa Madini Doto Biteko akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya PRNG Minerals
Ltd kutoka Marekani Rocky Smith kushoto kwa Waziri. Smith alimtembelea Waziri
ofisini kwake jijini Dodoma kwa mazungumzo akiwa ameambatana na Mkurungenzi wa
Maendeleo wa Kampuni hiyo Lucas Stanfield wa kwanza kulia, na wa kwanza kushoto
ni Mkurugenzi wa huduma za sheria Wizara ya Madini Edwin Igenge.
Waziri wa Madini Doto Biteko amekutana na
kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya PRNG Minerals Ltd, ya
Marekani, Rocky Smith na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni hiyo Lucas
Stanfield ofisini kwake Jijini Dodoma.
Watendaji hao wapo nchini kwa ziara ya kawaida ya
kikazi ya siku tano ambapo waliomba kukutana na Waziri wa Madini.
Pamoja na mambo mengine, kampuni hiyo inakusudia
kuwasilisha taarifa juu ya hali na Maendeleo ya soko la dunia kwa Madini ya
Rare Earth Elements na kuzungumzia hatua iliyofikiwa kwa ombi la leseni ya
uchimbaji Mkubwa wa madini hayo.
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Biteko
amesema wizara iko tayari kuipokea kampuni husika nchini baada ya
kukamilika kwa taratibu kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu Rocky Smith, amesema
kuwa, amefurahishwa na ushirikiano unaooneshwa na wizara na kuahidi
kuanza shughuli za uchimbaji mara baada ya kukamilika kwa taratibu.
XXX XXX XXX XXX
Caption
Waziri
wa Madini Doto Biteko akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya PRNG Minerals
Ltd kutoka Marekani Rocky Smith kushoto kwa Waziri. Smith alimtembelea Waziri
ofisini kwake jijini Dodoma kwa mazungumzo akiwa ameambatana na Mkurungenzi wa
Maendeleo wa Kampuni hiyo Lucas Stanfield wa kwanza kulia, na wa kwanza kushoto
ni Mkurugenzi wa huduma za sheria Wizara ya Madini Edwin Igenge.
Waziri
wa Madini Doto Biteko akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya PRNG Minerals
Ltd kutoka Marekani Rocky Smith kushoto kwa Waziri. Smith alimtembelea Waziri
ofisini kwake jijini Dodoma kwa mazungumzo, wa kwanza kushoto ni Ali Ali,
Kamishna Msaidizi Uendelezaji Migodi na Madini Wizara ya Madini, anaefuatia ni
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Wizara ya Madini Edwin Igenge.
0 comments:
Post a Comment