METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, February 18, 2019

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS IKUNGI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Uliyampti tayari kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Uliyampiti, Ikungi ambapo mradi huo utawanufaisha wakazi 2628. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua maji kama ishara ya uzinduzi wa huduma ya maji katika kijiji cha Uliyampiti, Ikungi ambapo mradi huo utawanufaisha wakazi 2628. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu (kushoto), Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi wakifurahia mara baada ya Makamu wa Rais kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Uliyampiti ambapo mradi huo wa maji utawahudumia wakazi 2628. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Tano imetekeleza kwa asilimia kubwa mambo yaliohaidiwa kwenye ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji utakaohudumia wakazi zaidi ya 2600 wa kijiji cha Ulyampiti, wilayani Ikungi mkoa wa Singida.

Ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani Singida, Makamu wa Rais ametoa agizo kwa Wizara ya Maji kuhakikisha katika mpango wa visima 20 wilayani Ikungi kimoja kichimbwe kijiji cha Mang’onyi.

Pamoja na mambo mengine Makamu wa Rais alitembelea zahanati ya Mang’onyi na kituo cha afya cha Ihanja na kujionea maboresho mbali mbali ikiwa pamoja na kufungwa mashine mpya ya upasuaji.

Akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Ihanja Madukani Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa bima ya afya kwa wananchi hao ikiwa na kuzitaka mamlaka husika kutoa elimu ya kutosha ili kila mwananchi aelewe mpango wa Serikali wa Bima kwa wote.

Aidha Makamu wa Rais amewataka wakazi wa Ihanja kutoruhusu mimba za utotoni kwani zinawanyima fursa ya mabinti wao kuja kuwa viongozi na wataalam wa badae, pia aliwasihi wananchi kuacha kukeketa mabinti kwani ukeketaji una athari nyingi zikiwemo vifo wakati wa kujifungua.

Makamu wa Rais amechangia mabati 200 kuunga mkono juhudi za Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi.

Wakati huohuo Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe. Elibariki Kingu amesema Chama na Serikali ni kitu kimoja kwani wanashirikiana katika kila jambo la kuleta maendeleo kwa wananchi ambapo ilani ya uchaguzi imetekelezwa kwa kiwango kikubwa. 
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com