Naibu waziri wa maji Juma Aweso ametoa wiki tatu kwa kampuni ya mavonoa’s kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa Sawala uliopo jimbo la Mufindi kusini katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
NAIBU waziri wa maji Juma Aweso akimbana mkandarasi wa kampuni ya mavonoa’s kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa Sawala uliopo jimbo la Mufindi kusini katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
NAIBU waziri wa maji Juma Aweso
ametoa wiki tatu kwa kampuni ya mavonoa’s kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa
mradi wa maji wa Sawala uliopo jimbo la Mufindi kusini katika wilaya ya Mufindi
mkoani Iringa.
Akizungumza mbele ya
wananchi,wabunge na wafanyakazi wa halmashuri hiyo,waziri Aweso alisema kuwa
amekuwa akipokea malalamiko mengi ya mkandasi huyo ambaye amekuwa hana
mahusiano mazuri na viongozi wa halmashauri hiyo.
“Mimi niseme ukweli nakupa wiki
tatu kuhakikisha unamalizia ujenzi wa mradi wa maji wa Sawala la sivyo utaniona
mbaya na mimi ni mkali kweli kwa wakandasi wamepewa kazi na serikali na
wanashindwa kutekeleza mradi kama ambavyo mkabata ulisema hivyo nakupa wiki
tatu kuhakikisha wananchi wanapata maji” alisema Aweso
Aweso alisema serikalia ya
awamu ya tano haita kubari kumuanda mkandarasi yeyote Yule aliyepewa kazi na
serikali anashindwa kukamilisha mradi wakati fedha amepewa,mkandarasi huyo
atachukuliwa hatua za kisheria haraka sana kwa kuwa saizi hakuna mtu kutumia
vibaya pesa za serikali kama ilivyokuwa huko nyuma.
“Walizoea kuzichezea pesa za
serikali miaka ya huko nyuma kwa sasa hakuna mkandarasi tayeweza kuichezea
serikali ya awamu hii kwa kuwa sisi wateule wa Rais wetu Dr John Pombe Magufuli
hakuna anayekubari kutumbuliwa kisa wakandarasi kufanya vibaya kwenye miradi
waliyopewa” alisema Aweso
Aidha naibu waziri Aweso
aliwatoa hofu viongozi wa halmashuri ya wilaya ya Mufindi kuhusu mkandarasi
huyo kuwa akishindwa kutekeleza mradi huo ndani ya wiki tatu hizo basi sheria
itachukua mkoando wake.
“Mkuu wa
wilaya,mbunge,mkurugenzi na mwenyekiti wa halmashauri niwahakikishieni kuwa
nitatakuja tena tarehe mbili mwezi wa tatu hapa kuja kuangalia kuwa huu mradi
umefikiwa wapi na makubariano yetu ameyatekeleza mkandarasi huyu” alisema Aweso
Awali mkuu wa wilaya ya Mufundi
Jamhuri William alimueleza naibu waziri kuwa mkandarasi huyoamekuwa anaidharau
serikali kwa kuwa mara kwa mara ameandikiwa barua na serikali ya wilaya lakini
hajawahi kujibu hata mara moja kitendo kinachoashiria dharau.
“Huyo mkandarasi amekuwa
anatusumbua sana maana tunamuita mara kwa mara hataki kuitika wito wetu hivyo
hizo ndio dharau kubwa kiasi kwamba anashindwa hata kuendelea kutekeleza mradi
huu ambao wananchi wanategemea kuwa mkombozi wao” alisema Jamhuri William
Mkuu wa wilaya alisema kuwa
atamkamata na kuwa ndani mkandarasi huyo kwa kuwa anachelewesha kuteleza mradi
huo wa maji na kusababisha wananchi kuichukia serikali kwa kusema kuwa wametoa
ahdi hewa kitua ambacho sio kweli.
“Mheshimiwa naibu waziri hapa
Sawala tunashindwa hata kufanya mikutano ya hadhara kwa ajili ya huu mradi wa
maji ambao mwazoni wananchi walijenga imani kubwa wakati wa kusainiana mkataba
wa kutekeleza mradi huu” alisema Jamhuri William
Akitoa malalamiko hayo
mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi Festo Mgina alimwambia naibu
waziri wa maji Juma Aweso kuwa hamhitaji tena huyo mkandarasi kwa kuwa amekuwa
kikwazo cha kuleta maendeleo ya wananchi kwa kushindwa kutekeleza mradi huo wa
maji.
“Huyu kwetu ni kero kubwa mno
mheshimiwa naibu waziri wa maji,sisi kama halmashauri hatupo tayari kufanya
kazitena na huyu mkandari kwa ujeuri wake na kushindwa kuiheshimu sekali ya
wilaya kwa kushindwa kumtua ndo mwanamke” alisema
Nao baadhi ya wananchi
walijitokeza hapo walimwambia naibu waziri kuwa mkandarasi huyo hafanyi kazi
ipasavyo kwa kuwa amesikia waziri unakuja ndio na yeye ameanza kazi jana tu ya
kukarabati tenki hili la maji ili ukifika uone kama yupo anafanya kazi wakati
sio kweli.
Hata hivyo naibu waziri Juma
Aweso alimalizia kwa kusema kuwa ifikapo tarehe mbili mwezi wa tatu mradi huo
uwe umekamilika na wananchi waweze kupata maji na kufanikisha adhima ya Rais ya
kumtua ndoo mwanamke.
0 comments:
Post a Comment