Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo
amewataka watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi, kuhakikisha kila
mtumishi kwa nafasi yake na majukumu yake anashirikishwa katika kutatua
changamoto za wananchi ikiwemo elimu, afya, maji na kilimo pamojana
kushirikiana na wananchi kutatua chnagmoto hizo.
Amesema kuwa ili kutatua hayo halmashauri
inapaswa kuongeza vyanzo vya mapato ikiwemo kuzidisha malengo ya makusanyo kwa
mwaka ili kuweza kukabiliana na changamoto anazokuwa anasomewa kila anapofanya
ziara katika shule mbalimbali za halmashauri na kumuomba achangie kutatua
changamoto zao.
“Mpige hesabu zote muwarudishie huko jamii
ili jamii iguswe kwamba alaa! Kumbe kuna changamoto kubwa sana zisingoje sisi
viongozi ambao pengine hatuna nafasi ya kuzunguka sekondari zote, lakini kama
tutafanya hivi tutaondoa changamoto zote hizi na matatizo na haya yote
mliyoyasema yako chini ya uwezo wenu, sio mambo ya mkuu wa mkoa haya, ni mambo
ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi, kata na vijiji vyenu, kama ni
“support” tunatoa ya kuhamasisha,naweza kusema nanunua bati mbili tatu, je,
ninatatua matatizo yote hayo?”Alibainisha.
Ameongeza kuwa kazi ya shule ni kuandaa
taarifa nzuri na kuikabidhi kwa watendaji wa halmashauri kuanzia Mtendaji wa
kata na vijiji pamoja na viongozi wa kisiasa akiwemo diwani wa kata husika ili
taarifa hizo ziwafikie wananchi watambue kupitia vikao vya kamati ya maendeleo
ya kata ambao ni mfumo mzuri uliowekwa na serikali katika kutambua changamoto
na kuzitatua.
Ameyasema hayo baada ya kupokea taarifa ya
shule ya sekondari Chala, iliyopo kata ya Chala Wilayani Nkasi na mkuu wa shule
hiyo Fatma Mchomvu aliyemuomba kufanya harambee ya haraka kutoka kwa msafara
alioambatana naoi li kuweza kukarabati nyumba ya “Matron” ambapo hadi
wanafikisha ombi hilo waalimu walikwishajichangisha shilingi 50,000/-.
“Walimu wamejitolea kuchangia 50,000/-
kusaidia kukarabati nyumba moja ya mwalimu ya “matron” kwasababu kule wanafunzi
wako peke yao hakuna ulinzi kwahiyo nao wakaomba kupitia msafara wako, na wewe
ndio kiongozi wetu tupate harambee ya haraka ili angalau tuanze kufanya
ukarabati wa jengo hilo ili angalau wanafunzi wawe salama kwasababu wanakaa
mbali na hakuna mlezi wa kukaa nae kule,” Alifafanua.
0 comments:
Post a Comment