Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka
wananchi wa Kata ya Paramawe yenye vijiji vitatu vya Lyazumbi, Paramawe ‘A’ na
‘B’ kuchangia shule moja ya msingi huku shule hiyo ikiwa na upungufu wa
madarasa ya kuwahifadhi wananfunzi 1400 wa shule hiyo iliyopo wilayani Nkasi.
Amesema kuwa umefika wakati wa kila Kijiji katika
kata hiyo kuhakikisha wanaanza ujenzi wa shule shikizi ili kuweza kuisaidia
mzigo wa wananfunzi uliopo katika shule hiyo mama iliyopo katika Kijiji cha
Paramawe ‘A’ na hatimae shule hizo shikizi zitakazoanzishwa katika vijiji hivyo
ziendelezwe na kusajiliwa na kuwa shule kamili.
Ameyasema hayo wakati alipoitembelea kata hiyo ili
kujionea maendeleo ya elimu ya shule ya msingi ambapo Kijiji cha Lyazumbi
tayari kimeshajenga madara matatu yaliyokamilika pamoja na vyoo na ofisi ya
walimu huku Kijiji cha paramawe ‘B’ kikikosa shule hiyo shikizi na hatimae
kuwapeleka Watoto wa katika shule ya msingi Paramawe ‘A’.
“Muanze kujipanga sasa hivi, Mkurugenzi tuma watu
waje wakae huku waone namna gani ya kuwasaidia hivi vijiji vitatu namna gani ya
kuondokana na changamoto hii ya msongamano ya Watoto kwa kuhakikisha kwamba
kila Kijiji kinakuwa na shule yake ya msingi na kwa kuanzia wawe na shule
shikizi, weka mkazo mkubwa kumaliza ile shule ya msingi Lyazumbi na isajiliwe
na hawa paramawe ‘B’ watafute eneo la kujengea shule hiyo,” Alisema
Aidha, katika kubainisha vigezo vya shule ya msingi
kukamilika na kuweza kusajiliwa, kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Nkasi Missana Kwangula alivitaja vigezo vinne vinavyopelekea shule ya msingi
kusajiliwa na kufafanua kuwa vigezo hivyo vimewekwa baada ya Wizara ya Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kubaini kuwa shule nyingi
zikianzishwa kama shikizi na kusajiliwa huwa haziendelezwi na wananchi na hivyo
kuupa mzigo serikali.
“Sasa hivi ili shule ya msingi isajiliwe lazima iwe
na vitu vya msingi vinne, cha kwanza vyumba visipungue saba kwa maana ya darasa
la kwanza mpaka la saba na cha pili kuwe na walau nyumba moja ya mwalimu
kwasababu mwalimu mkuu lazima akae shuleni, lakini cha tatu lazima kuwe na vyoo
vya makundi matatu vyoo vya wanafunzi wavulana na wasichana na vyoo vya walimu
na cha mwisho ni viwanja vya michezo na hasa mpira wa miguu na “netball””,
Alisema.
Shule Shikizi ya Kijiji cha Lyazumbi ina wanafunzi
375 wa darasa la kwanza hadi la tatu hali iliyomelekea Mtendaji wa Kijiji hicho
Elizabeth Alex kuomba msaada wa nguvu za wananchi, serikali pamoja na wadau wa
elimu nchini kusaidia ujenzi wa kumalizia shule hiyo.
0 comments:
Post a Comment