Katika hali ya kuupendezesha mji wa Sumbawanga Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameishauri wizara ya kilimo nchini kuona
namna ya kuhamisha mradi wa ujenzi wa vihenge kutoka katikati ya mji wa
Sumbawanga na kuhamishia katika eneo maalum lililotengwa na Halmashauri ya
Manispaa ya Sumbawanga kwaajili ya ujenzi wa maghala na viwanda ili kuutanua
mji na kujenga vihenge hivyo kwa nafasi.
Amesema kuwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula
(NFRA)tayari wamekwishanunua eneo la ekari 24.6 lenye thamani ya shilingi
298,938,000 lililopo katika eneo maalum lililotengwa kwaajili ya viwanda
vidogo, maghala na hotel lililopo Kijiji cha Kanondo, Kata ya Ntendo, Manispaa
ya Sumbawanga ambapo mpaka sasa viwanja vilivyouzwa katika eneo hilo ni
asilimia 35.
“Sisi tungependa kama mkoa wa Rukwa eneo hili
liwekezwe, kwasababu tuna uchumi wa kati wa viwanda, lakini sasa naona bado
tunapenda maeneo yet utu, sasa huku nani atakuja aendeleze? Kwakweli huu mradi
uje kujengwa huku ntashauriana na wizara ya kilimo..Mh. Waziri..tuone namna ya
kuleta huku, kwasababu hapo mnapotaka kujenga ni eneo dogo” Alisema.
Ameyasema hayo alipotembelea eneo hilo maaluma la
uwekezaji wa maghala lililililonunuliwa na NFRA miaka miwili iliyopita huku likiwa
limeachwa wazi bila ya matumizi yoyote.
Kwa upande wake Kaimu meneja wa NFRA Mkoa wa Rukwa
James Marwa alisema kuwa mradi wa vihenge ulianza kabla ya kununuliwa kwa eneo
hilo, hivyo ili kuhamisha mradi huo lazima eneo hilo jipya lipimwe upya.
Nae Afisa Mipango miji wa Manispaa ya Sumbawanga
Thadeo Maganga amesema kuwa hatachoka kuendelea kuwahamasisha wadau mbalimbali
kufika katika eneo hilo ili kuona umuhimu wake na kuweza kuwekeza kwa maslahi
ya Manispaa, Mkoa nan chi kwa ujumla.
Ujenzi
huo wa Maghala na Vihenge vya kisasa (Silos) utajengwa katika maeneo nane ya
kanda saba za wakala ambapo ujenzi huo utaongeza uwezo wa kuhifadhi mahindi
kutoka Tani 251,000 za sasa hadi Tani 700,000 ifikapo mwaka 2025.
Mradi
huo wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi umeanza kujengwa katika Manispaa ya Songea
(Ruvuma), Dodoma, Mpanda (Katavi), Makambako (Njombe), Mbozi (Songwe),
Sumbawanga (Rukwa), Shinyanga Mjini (Shinyanga), na Babati (Manyara) ambapo
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Poland zilisaini mkataba wa mkopo wa masharti
nafuu Septemba 2015 wa Dola milioni 55 sawa na sh. bilioni 124, kwa ajili ya
ujenzi wa mradi huo, ambao utaongeza uwezo wa hifadhi ya chakula.
0 comments:
Post a Comment