Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpwapwa Paul Sweya na Mkuu wa Idara ya Ardhi Anderson Mwamengo alipofanya ziara kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi katika halmashauri za mkoa wa Dodoma.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kongwa alipokutana na watendaji wa sekta ya ardhi katika wilaya hiyo wakati wa ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi katika halmashauri za mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deo Ndejembi akimuongoza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula kuelekea Masijala ya Ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Kongwa alipofanya ziara kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi katika halmashauri za mkoa wa Dodoma. Katikati ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt. Omar Nkullo.
Na Munir Shemweta, DODOMA
NaibuWaziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula ameshangazwa na halmashauri za wilaya
ya Mpwapwa na Kongwa mkoani Dodoma kushindwa kuwafikisha katika Mabaraza ya
Ardhi na Nyumba wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi pamoja na baadhi yao
kupelekewa ilani za madai.
Dk Mabula ameziagiza halmashauri hizo
mbili kuhakikisha zinawafikisha wadaiwa hao katika Mabaraza ya Ardhi kwa hatua
zaidi ambapo alielezea kuwa huko maamuzi yake ni mawili ambapo mdaiwa anatakiwa
kulipa ama kunyanganywa miliki yake kufidia deni.
Naibu Waziri wa Ardhi alitoa agizo hilo
jana alipozitembelea wilaya hizo mbili ikiwa ni mfululilzo wa ziara zake
kutembelea halmashauri mbalimbali kwa nia ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya
serikali kupitia kodi ya ardhi.
Kwa mujibu wa Dkt Mabula, halmashauri
hizo zina wamiliki wengi wa viwanja wasiolipia kodi ya ardhi na hivyo kuzifanya
kudai kiasi kikubwa cha fedha lakini idara za ardhi zinashindwa kuwachukulia
hatua jambo linaloikosesha serikali mapapto.
Naibu Waziri wa Ardhi alisema,
halmashauri ya wilaya ya Kongwa inadai jumla ya shilingi milioni 152 kutoka kwa
wamiliki wasiolipa kodi huku ile ya Mpwapwa ikidai milioni 128,013,696.90.
Afisa Ardhi Msaidizi wa Halmashauri ya
wilaya ya Kongwa Anjelina Ndemera alisema halmashauri yake pamoja na kuwa na madeni
kutoka kwa wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi lakini haikuweza kutoa ilani za
madai kwa wadaiwa hao.
Kwa upande wa wilaya ya Mpwapwa, Mkuu
wake wa Idara Anderson Mwamengo alisema halmashauri hiyo ina wadaiwa sugu wa
kodi ya pango la ardhi mia tatu na thelathini ambao wameandikiwa na
kukabidhiwa ilani hizo.
Dkt Mabula alisema, pamoja na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kuhimiza suala la kulipa
kodi na Wizara ya Ardhi kujitahidi kusaidia suala hilo lakini halmashauri
hazifanyi jitihada zozote katika kukusanya maduhuli ya Serikali kupitia kodi ya
ardhi.
‘’Kila siku inaelezwa pelekeni ilani za
madai ya kodi ya ardhi kwa wamiliki lakini hakuna ufuatiliaji wowote unaofanywa
na watendaji wa sekta ya ardhi jambo linalorudisha nyuma jitihada za serikali
ya awamu ya tano kukusanya maduhuli ya serikali.
Naibu Waziri wa Ardhi aliziagiza
halmashauri hizo mbili kufikia tarehe 31 Machi 2019 watendaji wake wa sekta ya
ardhi wawe wamewafikisha katika Baraza la Ardhi wadaiwa wote waliopelekewa ilani
za madai.
Aidha, Dkt Mabula ameitaka idara ya
ardhi kuhakikisha orodha ya wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi waliopewa ilani
za madai inafikishwa katika kila kikao cha kamati ya Uchumi na Mazingira vya
kila robo mwaka ya Baraza la Madiwani katika kila halmashauri lengo
likiwa kuitaka kamati husika kuelewa suala hilo na kufanya ufuatiliaji.
0 comments:
Post a Comment