Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akipita katika moja ya maeneo ya ujenzi wa ofisi katika Mji wa Serikali wa Mtumba mkoani Dodoma alipokwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi zinazosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).Wanaomfuatia kwa nyuma ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba Dkt Sophia Kongela na Mkurugenzi Dkt Maulid Banyani.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akiangalia shimo la choo katika wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi za Serikali katika Mji wa Serikali Mtumba mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akiangalia madirisha ya nondo ambayo yako tayari kupachikwa wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi za serikali katika eneo la Mtumba. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa Dkt Maulid Banyani.
Na Munir Shemweta, DODOMA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline
Mabula amechochea kasi ya ujenzi wa ofisi za serikali katika eneo la Mtumba
mkoani Dodoma unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Kasi hiyo inatokana na ziara za mara kwa mara zinazofanywa na
Naibu Waziri huyo wa Ardhi katika eneo hilo kwa nia ya kuhakikisha ujenzi wake
unakamilika katika muda uliopangwa.
Akiambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa
.Dkt Sophia Kongela pamoja na Mkurugenzi wa Shirika Dkt Maulid Banyani jana,
Naibu waziri Mabula alijionea maendeleo makubwa ya ujenzi huo ambapo sasa
umefikia hatua ya kuezeka.
Mbali na kufikia hatua hiyo, kazi nyingi katika ujenzi huo
zinaenda kwa pamoja kama vile kuweka njia za umeme, tiles, utengenezaji
madirisha ya nondo pamoja na mashimo ya choo jambo linaloonesha
Shirika limejipanga kukamilisha kazi mapema tofauti na makampuni mengine ya
ujenzi yanayofanya kazi kwenye eneo la Mtumba.
Kampuni ya Ujenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa katika eneo hilo
la Mtumba inajenga majengo ya ofisi nne za Wizara ya Ardhi Nyumba na
Maenendeleo ya Makazi, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Nishati pamoja
na Wizara ya Fedha na Mipango.
Akizungumza baada ya kukagua kwa mara ya pili ujenzi wa
ofisi hizo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Mabula
alisema kasi inayooneshwa na Shirika la NHC katika ujenzi huo ni ishara tosha
kuwa shirika hilo kupitia kampuni yake ya ujenzi lina uwezo mkubwa wa kujenga
majengo kwa haraka na yenye viwango.
Alisema, hata kama ujenzi wa ofisi zinazosimamiwa na shirika hilo
katika eneo la Mtumba utachelewa kidogo lakini ucheleweshaji huo utatokana na
MHC kutaka kujenga majengo ya uhakika na yenye ubora unaotakiwa.
Dkt Mabula ameendelea kutoa sifa kwa Ofisi ambazo majengo yake
yanasimamiwa na shirika la Myumba la Taifa kutokana na ukaribu inaouonesha katika
kipindi chote cha ujenzi kwa nia ya kuwa na majengo yanayokidhi mahitaji ya
Wakala wa Ujenzi Tanzania (TBA) na ofisi husika kwa kuwa mawazo ya pande zote
yatakuwa yamejumuishwa katika kutekeleza ujenzi huo.
0 comments:
Post a Comment