METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, January 7, 2019

MBUNGE SERENGETI ATEKELEZA ILANI YA CCM KWA VITENDO WANANCHI WAPONGEZA




Na Maiko Luoga

Mbunge wa Jimbo la Serengeti Mkoani Mara Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Mh. Marwa Ryoba Chacha January 03 Mwaka huu 2019 Alifanya Ziara ya Kikazi katika Kata ya Matare Ili Kusikiliza Kero za Wananchi na Kuzitafutia Ufumbuzi.

Ziara hiyo ya Kikazi Iliyofanywa na Mh. Marwa Chacha Ilihudhuriwa na Wajumbe wa Kamati ya maendeleo ya kata ya Matare KAMAKA wakiongozwa na Diwani wa Kata hiyo Mh.Nyangi, Wananchi wa Matare Pamoja na Vingozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Ambao walishuhudia Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa Vitendo.

Akizungumza na Mwandishi wetu Kwa Njia ya Simu Mbunge huyo wa Jimbo la Serengeti Mkoani Mara Mh. Marwa Chacha Alisema Kuwa Mkutano Mkubwa wa Hadhara Ulifanyika katika Kitongoji cha Matare Chenye Shule ya Msingi ambayo Choo chake Kipo katika Hali mbaya hivyo Mbunge huyo Aliamua kuwachangia wananchi fedha Kiasi cha Tsh. 3,000,000/=ili Kukamilisha Ujenzi wa Choo hicho cha Wanafunzi.

Aidha Mh. Chacha Alitoa kiasi cha Tsh.2,000,000/= kwa ajili ya ukamilishaji wa darasa Moja na ofisi ya walimu Katika Shule ya Msingi Igina Ujenzi ambao wananchi waliuanzisha Kwa nguvu zao wenyewe lakini Haukufika Mwisho Hivyo Pesa hiyo itawasaidia Kukamilisha Ujenzi Huo Pia Katika Shule Mpya inayoanzishwa katika Kitongoji cha Kegonga Mbunge huyo Alikabidhi Kiasi Cha Tsh.5,000,000/= Ili kuwaunga Mkono wananchi Kwaajili ya ukamilishaji wa Majengo Mawili ya madarasa.

Kuhusu Ushirikiano wake na Wananchi Mh. Marwa Ryoba Chacha Mbunge wa Serengeti Alieleza Bayana kuwa Ushirikiano Ni mkubwa Hali ambayo Itazaa Matokeo Mazuri Kwa Chama cha Mapinduzi CCM Jimboni kwake katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Utakaofanyika Mwaka huu 2019 Kwakuwa Jimbo Hilo ni la CCM Tangu yeye Akiwa Chadema Akisema kuwa Hata waliompigia Kura Akiwa Chadema ni Wanachama wa CCM.

"Nikujulishe Ndg. Mwandishi wa Habari kwamba Kwaasili Serengeti ni Jimbo la CCM Hata mimi wakati nikiwa Chadema walionipigia kura ni Wana CCM Ndio maana wakati Nimeamua Kurudi CCM Wananchi walifarijika Sana lakini Walihuzunika kama kumetokea Msiba wakidhani Sitarudi tena Bungeni Kutokana na Namna ninavyofanya Kazi kwakushirikiana nao Na walipoona Nimegombea Tena Kupitia CCM Walinichagua kwa Kishindo Kikubwa Hivyo Nasema Vitongoji na Vijiji vyote Mwaka huu Vitaenda CCM Naomba hata Mh. Rais Alitambue hilo".Alisema Mh. Chacha Mbunge wa Serengeti.

Katika hatua Nyingine Mbunge huyo Amesema kuwa CCM yasasa chini ya Nwenyekiti wake wa Taifa na Rais wa Tanzania Ndg. John Magufuli Imesimama Imara katika Kutetea Wananchi Ndio maana Watanzania Wanaendelea Kukiamini Chama hicho Nakuongeza Kuwa Baada ya Bunge Mwezi February Mwaka Huu Atafanya Ziara ya Kikazi katika Kata zote za Jimbo lake la Serengeti Kuzungumza na Wananchi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com