Ndugu Fred Kafeero akimkabidhi Naibu Waziri wa Kilimo baadhi ya machapisho yanayoonyesha mikakati ya FAO
Mheshimiwa Innocent Bashungwa akimueleza muwakilishi wa FAO nchini mipango ya Serikali ya awamu ya tano katika kuinua kilimo
Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa akizunguza na mwakilishi wa Shirika laUmoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) Ndugu Fred Kafeero na msaidizi wa mwakilishi huyo Ndugu Charles Tulahi katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam
Shirika la Umoja wa
Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) limeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali
ya Tanzania katika kuiinua sekta ya kilimo nchini. Hayo yamesemwa na Ndugu
muwakilishi wa Shirika hilo nchini Ndugu Fred Kafeero alipokutana na Naibu
Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa katika ofisi za FAO jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho
Ndugu Kafeero alieleza namna ambavyo shirika hilo limekuwa mstari wa mbele
kushirikiana na serikali katika kutunga sera na kuandaa mikakati yenye lengo la
kuhakikisha Tanzania inasonga mbele katika kilimo. Amesema FAO kwa miaka ya
karibuni imefanya kazi kwa ukaribu na Shirika la Takwimu Tanzania (NBS) kwa
kulijengea uwezo wa ndani unaoisaidia pia serikali katika ufuatiliaji wa bei ya
mazao nchini.
Nae Naibu Waziri wa
Kilimo Innocent Bashungwa alimueleza muwakilishi huyo mpango wa Serikali ya
awamu ya tano wa kuorodhesha wakulima wote nchini ili kuweza kupanga vizuri
kuhakikisha kila mkulima anapata huduma muhimu zitakazomsaidia toka hatua za
uandaaji shamba mpaka masoko, na kuiomba FAO kama mdau muhimu wa kilimo kuipa
Serikali ushirikiano ambapo Ndugu Kafeero aliahidi kulifanyia kazi ombi hilo.
Aidha, Naibu Waziri
Bashungwa ameomba IFAD (shirika tanzu la FAO) isaidie Serikali kwa kushirikiana
na Benki ya Kilimo nchini kuwapatia wakulima nchini kupata mikopo ya
riba nafuu, kusaidia taasisi za utafiti wa kilimo nchini, kujenga uwezo wa
kuzalisha mbegu za mazao ya kimkakati na mchanganyiko, kujenga maghala ya
kuhifadhi mazao ili kupunguza hasara wakati wa mavuno shambani (post harvest
losses) na kuwajengea uwezo maafisa ugani nchini kufundisha kilimo cha tija kwa
wakulima nchini.
Mwakilishi wa FAO
nchini amekubaliana na Naibu Waziri Bashungwa kufanyika kikao mwezi Februari
2019 cha Wizara ya Kilimo, FAO na mashirika mengine ya kimataifa yanayohusika
na kilimo nchini kujadili vipaumbele tajwa ili kuijengea uwezo Wizara wa kuweza
kuihudumia sekta ya kilimo nchini ili iendelee kukua na kutimiza azma ya
Serikali ya awamu ya tano ya kufikia uchumi wa kati.
0 comments:
Post a Comment