MAMLAKA
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imeendelea kuwa mstari wa mbele katika
kufanikisha shughuli mbali mbali za jamii, kwa kutoa misaada yenye tija.
Hilo
limekuwa bayana leo tarehe 12 Disemba, 2018 kwenye Kijiji cha Makumbosho Jijini
Dar es Salaam, ambapo TAA imetoa msaada wa fulana 100 kwa ajili ya kufanikisha
Tamasha la Utamaduni la Chato linalotarajiwa kufanyika tarehe 22 Disemba, 2018
katika Uwanja wa Mazaina Chato.
Akizungumza
katika Mkutano wa waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na
Utawala wa TAA, Bw. Abdi Mkwizu amesema Mamlaka ina wajibu mkubwa wa kuunga
mkono shughuli za kijamii, kwa kutoa misaada ya mbalimbali.
“Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege Tanzania ina wajibu wa Kusimamia, kuendesha, kuboresha na kuendeleza
Viwanja vya Ndege Tanzania lakini pia mbali na kutoa huduma hizo tuna wajibu wa
kushiriki katika shughuli za kijamii, kwa wadau ambao wanatufanya sisi tuwepo,”
amesema Bw. Mkwizu.
Pia Bw.
Mkwizu amebainisha kwamba TAA inahudumia Viwanja 58 vilivyopo Tanzania Bara
chini ya serikali, hivyo ni wajibu wao kushiriki katika shughuli za kusaidia
jamii sehemu yeyote ile kulingana na uhitaji na bajeti iliyopo.
“Ikumbukwe
siku za hivi karibuni TAA tumeshirika katika kufanikisha Tamasha la Urithi Wetu
lililofanyika kuanzia Oktoba Mosi mpaka Oktoba 7, 2018 katika Kijiji cha
Makumbusho, tumetoa pia msaada wa Mafuta Kinga jua ya Ngozi kwa watoto wenye
ulemavu wa Ngozi katika baadhi ya shule hapa Dar es Salaam, lakini pia tarehe
24 Novemba mwaka huu tumekabidhi Shule ya Msingi ya Kisasa huko Bukoba inaitwa
Tumaini, na tunaamini itaongeza ufaulu
kwa wanafunzi huko Bukoba na hayo ni macheche kati ya mengi ambayo Mamlaka
inafanya kwa Jamii” amebainisha Bw. Mkwizu.
Akizungumza
kwa niaba ya Waziri Mkuu na niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Bw. Habbi Gunze
ameishukuru Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania kwa mchango wake kufanikisha
Tamasha la Utamaduni la Chato.
“Niwashukuru
sana Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania kwa mchango wao nap engine bila wao
hili la leo lisingeweza kufanikiwa. Utamaduni ndio uhai wa Taifa, kwa hiyo nchi
isipokua na Utamaduni nchi inakua sio hai, hivyo kwa Mchango huu wa kusaidia
hili nawapongeza sana TAA” amesema Bw. Gunze.
Naye
Mkurugenzi wa Chief Promotions ambaye ndie mratibu wa Tamasha hilo Bw. Amon
Mkoga amesema kwamba Tamasha litakuwa na mambo yote ya kiutamaduni ili kuenzi
asili ya Kitanzania.
“Kauli
mbiu ya Tamasha la Utamaduni la Chato inasema “Maendeleo ya Viwanda yasiache
Utamaduni nyuma” ambapo Tamasha hili ni maalum kwa ajili ya kuuenzi utamaduni
wa Mtanzania. Katika Tamasha hili kutakua na Vikundi mbalimbali vya Utamanduni.
Vikundi vya ngoma vitakuwepo kutoka Simiyu, Shinyanga, Geita, Mwanza, Tabora na
Chato wenyewe, hivyo tunawaomba wananchi mtusaidie kufikisha taarifa hizi kwa
watanzania” ameeleza Bw. Mkoga.
Tamasha
la Utamaduni la Chato ni tamasha kubwa la ngoma ambalo hufanyika kila mwaka nah
ii itakua ni mara ya tatu mfululizo likifanyika Chato mkoani Geita.
0 comments:
Post a Comment