Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (CCM)
ametoa shilingi Milioni 22 kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya soko la Mlango
Mmoja iliyoteketea kwa moto miezi mitatu iliyopita.
Mabula aliyasema hayo jana baada ya kuwatembelea wafanyabiashara
wadogo (machinga) katika soko hilo na kubainisha kwamba fedha hizo kutoka mfuko
wa jimbo zitasaidia ujenzi wa paa lote.
Mwenyekiti wa soko hilo, Jackson Kayoza alisema kulingana na
tathmini iliyofanyika, shilingi Milioni 98 zinahitaji kwa ajili ya ujenzi wa
sehemu iliyoungua moto hivyo alimshukru mbunge Mabula kwa mchango huo.
Mmoja wa machinga katika Soko la Mlango Mmoja ambaye pia bidhaa
zake zilitekeketea kwa moto, Isaack Julius, alisema mchango wa mbunge Mabula
uwe chachu kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kuhakikisha inakamilisha kiasi
cha fedha kinachohitajika ili ujenzi huo uanze mara moja.
Septemba 28, 2018 majira ya alfajiri, ajali ya moto ilizuka katika
Soko la Mlango Mmoja na kusababisha meza 83 za wajasiriamali, maduka 23 na vyoo
vitatu kuteketea ambapo hasara yake haikujulikana mara moja.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula
(katikati), akizungumza na wafanyabiashara wadogo (machinga) katika Soko la
Mlango Mmoja Jijini Mwanza.
0 comments:
Post a Comment