Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki (wa pili kushoto) akiambatana na Viongozi Waandamizi wa Wizara ya Madini
mara baada ya kufika katika eneo la ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Madini eneo la
Ihumwa jijini Dodoma.
Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki (wa tatu) wakitoka kukagua eneo la ujenzi wa jengo
la Wizara.
Muonekano wa moja wapo wa jiwe lililopo katika eneo la kujenga Jengo la
Wizara ya Madini.
Na
Rhoda James – Dodoma
Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki ameagiza Kampuni ya Mzinga Holding Co. Ltd
kukamilisha ujenzi wa Jengo la Wizara ya Madini ifikapo Januari 4 mwaka 2019.
Ametoa
agizo hilo jana tarehe 4 Desemba, 2018 alipofanya ziara ya kukagua eneo la
ujenzi wa ofisi za Wizara lililopo Ihumwa Jijini Dodoma akiambatana na viongozi
wengine waandamizi wa wizara.
Kairuki
alibainisha kuwa baada ya sikukuu za mwisho wa mwaka, viongozi wote watatakiwa
kuhamia katika eneo hilo kutokana na ukweli kuwa ifikapo Januari 4 jengo hilo litakuwa
limekamilika.
Aidha,
Waziri Kairuki ameshauri kuwa wakati wanaendelea na maandalizi mengine waendelee
na manunuzi ya vifaa, na vifaa hivyo lazima viwe vya viwango ikiwezekana
watumie dealers ambao ni wakubwa na wa uhakika.
Kwa
upande wake, Mhasibu Mkuu wa Wizara, Anthony Tarimo alisema kuwa pesa kwa ajili
ya ujenzi huo ipo, wao wanachohitaji ni kujua mkataba ukoje na guarantee ili
pesa kwa ajili ya ujenzi huo itolewe.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Issa Nchasi ameeleza kuwa
wamejiandaa kikamilifu ili kusimamia ujenzi wa Jengo hilo na atateua watu ambao
watafutilia kwa ukaribu shughuli za kila siku za ujenzi wa Jengo hilo.
Vile
vile, Mwakilishi wa Kampuni ya Mzinga Holding Co. Ltd, Mhandisi Hagai Mziray
amesema wataanza maandalizi ya ujenzi wa Jengo la Madini mapema tarehe 5
Decemba, 2018 na watafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kuwa wanakamilisha
ujenzi kwa wakati.
Mziray
ameongeza kuwa Kampuni yao inao uzoefu wa kutosha katika masuala ya ujenzi
kwani wamejihusisha na ujenzi wa majengo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Manispa
ya jiji Dodoma, Hosipitali ya Makole, Hosipital ya Mkoa wa Morogoro pamoja na
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi.
Kwa
sasa Wizara ya Madini inatumia Ofisi za Wakala wa Jiologia Tanzania (GST)
zilizopo Mjini Dodoma.
Captions
Pic 1
Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki (wa pili kushoto) akiambatana na Viongozi Waandamizi wa Wizara ya Madini
mara baada ya kufika katika eneo la ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Madini eneo la
Ihumwa jijini Dodoma.
Pic 2
Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki (wa kwanza) akiondoka eneo la ujenzi wa Jengo la
Madini mara baada ya kukagua eneo hilo ambalo linakhadiriwa kuwa na hekta 3-4.
Pic 3
Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki (wa pili kulia) akijadili jambo na Manaibu Waziri
wa Madini, Doto Biteko (kulia) na Stanslaus Nyongo (wa tatu kulia) na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Madini Saimon Msajila (kushoto) wengine katika picha ni
Viongozi mbalimbali wa wizara.
Pic 4, 5 na 6
Muonekano
wa eneo la ujenzi wa Jengo la Wizara ya Madini.
Pic 7
Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki (wa tatu) wakitoka kukagua eneo la ujenzi wa jengo
la Wizara.
Pic 8
Mkurugenzi
Msaidizi wa Utawala na rasilimali watu Nsajigwa Kabigi, akitoa maelezo kwa
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (katikati) kuhusu eneo la ujezi wa Ofisi ya
Madini.
Pic 9
Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki akijadili jambo na Mhasibu Mkuu wa Wizara, Anthony
Tarimo (wa pili) wakati walipokuwa wakikagua eneo la ujenzi wa Jengo wa Wizara
tarehe 4 Decemba, 2018.
Pic 10
Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki (wa tatu) akiwa na Viongozi Waandamizi wakati wa
ukaguzi wa eneo la ujezi wa Jengo la Madini tarehe 4 Decemba, 2018.
Pic 11
Muonekano
wa moja wapo wa jiwe lililopo katika eneo la kujenga Jengo la Wizara ya Madini.
0 comments:
Post a Comment