METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, November 19, 2018

YALIYOSEMWA NA SHAKA H. SHAKA KATIBU WA CCM MKOA WA MOROGORO KATIKA MAHAFALI YA KWANZA YA KIDATO CHA NNE MOROGORO OPEN SCHOOL

Shaka#  Nawashuru  walimu, wazazi na wanafunzi kwa mashirikiano yaliyopelekea kufanya vizuri sana katika mitihani ya mwaka 2017 ongezeni bidii, jitihada,  umoja na mashirikiano#

Shaka#  Sote tunafahamu ili Serikali iweze  kufikia malengo na  mafanikio  ni lazima iwe na muundo, mpangilio wa kisera, mfumo wa kioganaizesheni, uhamasishaji na mipango katika  kukuza elimu ya msingi, Sekondari na  vyuo vikuu inabopidi hujibadili kulingana na matakwa ya wakati#

Shaka#  Sote mashahidi kuwa Watanzania hawana shauku wala ndoto ya kutaka mabadiliko ya utawala kwa kutegemea wenye mawazo duni waliokosa dira na malengo huku serikali ya CCM ikijibadili, kimfumo na kisera kukidhi matakwa ya wakati katika sekta ya elimu#

Shaka #  Naipongeza  Serikali kupitia wizara ya elimu kwa kufanya mabadiliko ya kimfumo na kisera ili kukidhi mahitaji ya nyakati inayopelekea kutengeneza wahitimu watakao kimbizana na mazingira ya kiuchumi, kijamii na kisiasa kama ilivyoelekezwa katika ilani ya uchaguzi 2015/2020#

Shaka#  lazima tutambue kuwa juhudi zinazochukuliwa na serikali katika kuimarisha sekta ya elimu ni kubwa ikiwa ni pamoja na kuongeza budget ya wizara, mchango katika sekta binafsi katika kudahili wanafunzi wa vyuo vya ufundi, mafunzo na elimu ya ufundi sambamba na kusimamia sera ya elimu na mafunzo ya ufundi kama ilivyoelekezwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM#

Shaka#  Tofauti ya msingi ya viongozi wa  CCM na wengine ni kuwa wanajikita katika utundu unaoshikamaa na ubunifu wa masuala nyeti ya kisera na kimfumo kwa muktadha wa kupima mwelekeo wa kiuchumi, diplomasia yenye manufaa na mabadiliko ya kidunia kulingana na mahitaji ya wakati#

Shaka#  Serikali ya CCM chini ya uongozi wa Rais Magufuli itabaki madarakani ikiamini siasa ya ujamaa tokea zama za sera za uchumi hodhi na hata baada ya ujio wa soko huria na utandawazi , haishikilii ukale ikiwa mbele yake kunahitajika mabadiliko ya msingi#

Shaka# Anayefikiri Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea imekufa yeye mwenyewe hajielewi , serikali inaposomesha wanafunzi bure, kutafuta madawati, kulipa mishahara walimu, kujenga vyuo vikuu, kutafuta vifaa vya kufundishia, vitabu vya ziada na kiada, zahanati na hospitali ni utekelezaji chini ya siasa ya Ujamaa# 

Shaka#  Maisha ya watanzania kwa kiasi kikubwa ni ya kijamaa kwani kupendana kwao, kuheshimiana na kusaidiana kunatokana na kujengeka kwa fikra za ujamaa, umoja wa kitaifa bila kujali itikadi za kisiasa ama ubaguzi wa aina yoyote mwingine#

Shaka#  Leo hii kama utawahoji wananchi kumi watoe maoni kuhusu utawala wa Serikali ya Rais Dk John Magufuli, wanane watamtaja ni kiongozi bora Afrika huku wawili kati yao watakosoa bila ya kuwa na nguvu ya hoja kwa kigezo hicho Serikali ya hii inayongozwa na Chama Cha Mapinduzi bado inaheshimika sana#

Shaka#  Nawahimiza watanzania kujenga matumaini na matarajio katika sera za chama cha Mapinduzi kwani ndicho chenye uwezo, ushahidi na uhodari wa kutenda jambo lolote ambalo haliwezi kufanywa na wengine nje ya mfumo wa CCM#

Shaka#  Nawahimiza na kuwatia shime wanafunzi msome kwa bidii na wale waliohitimu watambue wana jukumu la kujiandaa vyema kutumia fursa zinazotolewa na serikali kujiendeleza ili kuweza kuja  kulikabili soko la ajira chini baadae#

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com