Waziri wa Madini Angellah Kairuki akieleza jambo. Kulia ni Mkuu wa MKoa wa Mara, Adam Malima na kushoto ni Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko
Waziri wa Madini Angellah Kairuki akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (kulia)
Sehemu ya Watendaji kutoka Wizara ya Madini, Uongozi wa Mkoa wa Mara wakifuatilia kikao hicho.
Na Asteria Muhozya, Mara
Waziri wa Madini Angellah Kairuki ameuagiza Wakala
wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kuvunja uongozi wa Mfuko wa Udhamini wa
North Mara ( Bodi ya Wadhamini na Menejimenti) kwa kuwa umeshindwa
kusimamia uendeshaji wa Mfuko kwa tija na kuandaa utaratibu mzuri
wa usimamizi wa Mfuko huo ambao utakuwa na manufaa kwa Taifa
.
Aidha, Waziri Kairuki amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya
Tarime kuruhusu fedha za Keng'anya Enterprises Ltd ( KEL) kuendelea kulipwa
hadi hapo vyombo vya uchunguzi vitakakapobaini na kuelekeza vinginevyo,
huku Mkuu wa Mkoa wa Mara akitakiwa kusimamia utekelezaji wa agizo hilo.
“Kwa kuwa Keng'anya
Enterprises iliomba kupata PL 303/95 kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu
zinazosimamia Sekta ya Madini, hivyo malipo ya mrabaha wa asilimia moja
yanayopokelewa kutoka kwenye mgodi kwa mujibu wa mkataba wake ni halali,”
alisisitiza Kairuki.
Waziri Kairuki alitoa maagizo hayo Novemba 21, ikiwa ni
utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Magufuli ambaye alielekeza kufanyika uchunguzi wa Mfuko wa North Mara Community
Trust Fund, baada ya baadhi ya wananchi wa Nyamongo Wilayani
Tarime kulalamika juu ya jamii kutofaidika na mfuko huo na badala yake
kunufaisha baadhi ya watu wachache.
Rais Magufuli alitoa maelekezo ya kufanyika kwa
uchunguzi wa mfuko huo wakati wa ziara yake Mkoani Mara tarehe 4 hadi 8
Septemba, 2018.
Mbali na agizo la kuuvunja uongozi wa mfuko, Waziri
Kairuki aliiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
kuwachunguza na kuwachukulia hatua za kisheria wajumbe wa bodi ya wadhamini,
menejimenti ya mfuko na yeyote atakayethbitika kujihusisha na ufujaji na
matumizi mabaya ya fedha za mfuko.
Pia, aliiagiza serikali ya Mkoa kukaa na wamiliki
wote wa leseni zilizopo ndani ya Mgodi ambao wanalipwa mrabaha wa asilimia 1
kuangalia mfumo bora ili nao wachangie kwenye mfuko sehemu ya fedha wanazopokea
kwa ajili ya maendeleo ya vijiji vnavyozunguka Mgodi wa North Mara.
Vilevile,
aliigiza TAKUKURU kuchunguza na kuwachukulia hatua za kisheria watumishi wote
watakaobainika kufanya ufujaji na ubadhirifu wa fedha za umma shilingi
214,000,000.
Maagizo
ya Waziri Kairuki yanatokana na yaliyobainika katika kamati iliyoundwa na
Wizara ya Madini baada ya kutolewa maelekezo ya kuchunguzwa kwa mfuko huo na
Rais Magufuli.
Waziri
Kairuki alisema miongoni mwa mambo
iliyoyabaini kamati hiyo ni pamoja na Kampuni
Tanzu ya North Mara Commercial Business Ltd tarehe 20 Aprili, kutoa kiasi cha
shilingi milioni 214,000,000 kwenda kwa DAS Tarime kwa ajili ya uwekezaji wa
kilimo cha miwa, ambapo katika taarifa yake, Waziri Kairuki alisema kuwa, fedha
hizo zilitokana na maombi yaliyowasilishwa na
Mkuu wa wilaya ya Tarime, ambazo hata hivyo, hazikuzingatia utaratibu wa
fedha za umma na manunuzi.
“
Kampuni Tanzu ilifunguliwa mwaka 2017 ambayo wana hisa wake ni North Mara
Community Trust Fund asilimia 99 na Bw., Robin Motengi Marwa asilimia 1,”
alisema Kairuki
Aliongeza kuwa, pia
ilibainika kuwa, wajumbe wa bodi ya wadhamini wamekuwa wakikopeshwa
fedha za mfuko kinyume na malengo ya uanzishwaji wa mfuko huo.
Pia, kamati hiyo
ilibaini kwamba, kati ya Mwaka 1990 hadi 1998, vijiji vya Nyangoto, Karende,
Kewanja, Genkuru na Nyamwanga viliwahi kumiliki leseni tano za uchimbaji (CTs).
Mwaka 1996, vijiji hivyo vilibadili leseni hizo kwa hiari yao na kuwa leseni ya
utafiti PL 370/96 na kisha kuihamishia kwenye Kampuni ya East African Gold
Mining Ltd (EAGM) na kisha kubadilishwa kuwa leseni ya uchimbaji wa kati (ML
17/96).
Halikadhalika, Waziri
Kairuki alisema kamati ilibaini kuwa,
North Mara Community Trust Fund ilianzishwa kwa makubaliano kati ya
Mgodi na kampuni ya KEL ya Mwaka 2004.
Mfuko huo ulisajiliwa Mwaka 2013 na kuanza kazi Mwaka 2015. Aliongeza kuwa,
wachangiaji pekee wa Mfulo huo ni KEL na Mgodi kwa kiwango cha sawa cha
asilimia 0.1 ya uzalishaji katika eneo la KEL.
“ Mfuko huo unaendeshwa
na wajumbe wa bodi inayoundwa na pande zote tatu yaani Mgodi, KEL na vijiji,
bodi inatakiwa kuwa na wajumbe wasiopungua watano.
Akizungumza kuhusu
malengo ya kuundwa mfuko huo, alisema kamati ilibaini kwamba mfuko ulianzishwa
kwa lengo l kutafuta shughuli zenye manufaa kwa jamii, kuhamasisha, kusaidia na
kuwezesha program na shughuli kwenye maeneo ya elimu, mafunzo, afya, uwezo
kilimo , maji na kupunguza umaskini kwa ujumla kadri ya wadhamini watakavyoona
inafaa.
Kwa upande wake, Mkuu wa
Mkoa wa Mara Adam Malima, alisema kazi hiyo ilifanyika kwa kipidi cha miezi
miwili na hivyo kumshukuru waziri na wote walioshiriki kukamilika maagizo hayp hayo ya kufanyika uchunguzi,
yaliyotolewa na Rais Magufuli.
0 comments:
Post a Comment