Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya
Mji wa Geita kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Novemba 27, 2018.
Kulia ni Mbunge wa Chato na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na kushoto
ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Geita wakimsikiliza Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa
Halmashauri hiyo, Novemba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Geita wakimsikiliza Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa
Halmashauri hiyo, Novemba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamewaagiza Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wahakikishe wanasimamia vizuri uwajibikaji na utowaji wa huduma kwa wananchi katika maeneo yao bila ya woga.
Kadhalika, Waziri Mkuu
amemtaka kila mtumishi wa umma nchini awajibike katika kufanya kazi kwa bidii
na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano haitowavumilia watumishi ambao ni wezi,
wabadhilifu, wavivu na haitosita kuwachukulia hatua.
Waziri Mkuu
aliyasema hayo jana jioni (Jumanne, Novemba 27, 2018)
alipozungumza na watumishi, viongozi wa mkoa, wilaya ya Geita na taasisi za
umma katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Mamlaka ya Mji Geita.
“Watumishi
fanyeni kazi kwa bidii na msitarajie kuundiwa tume pale mnapofanya vibaya,
ukiharibu kazi tunakushughulikia hapo hapo na huu ndio msimamo wa Serikali ya
Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli.”
Waziri Mkuu
aliwaeleza watumishi hao kuwa wanatakiwa wafanye kazi kwa kuzingatia sheria na
kanuni za kazi na pia watambue dhamana kubwa waliyonayo, ambayo ni kuwahudumia wananchi
wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Katika hatua
nyingine, Waziri Mkuu amewaagiza watumishi wa umma hususani
Wakuu wa Idara wahakikishe wanakuwa na kitabu cha Ilani ya Uchanguzi ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM) ili wapate muelekeo wa utekelezaji washughuli zao.
Waziri Mkuu
amesema kitabu cha Ilani ya uchanguzi cha CCM 2015/2020 kina maelekezo ya
utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo kila idara inatakiwa kuangalia
maelekezo yaliyotolewa kuhusu idara husika na kuyafanyia kazi.
Kwa upande wake
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel alimuhakikishia Waziri Mkuu
kwamba yeye kwa kushirikiana na viongozi wenzake watayafanyia kazi maelekezo
yote ambayo ameyatoa.
0 comments:
Post a Comment