Na; Mwandishi Wetu
Vijana
Nchini Wameaswa kushirikiana na Serikalini pamoja na wadau mbalimbali katika
mapambano dhidi ya mambukizi ya virusi vya UKIMWI na kwa kuepuka Tabia
hatarishi.
Akizungumza
wakati wa kilele cha wiki ya Vijna kilichofanyika leo Jijini Dodoma ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya Siku ya UKIMWI
Duniani itakayoadhimishwa kesho
Novemba Mosi 2018, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana Ajira
Mhe. Antony Mavunde amesema kuwa Vijana ni zaidi ya asilimia 68 ya nguvu kazi
ya Taifa hivyo ni vyema kundi hilo likachukua tahadhari katika kujikinga na
maambukizi ya mapya ya VVU.
"
Takwimu zinaonesha kuwa takribani watu elfu 81,000 huambukizwa Virusi vya
UKIMWI kila mwaka hapa nchini, hii ni sawa na takribani watu 6750 kwa mwezi na
kwa siku ni wastani wa watu 225 na katika maambukizi mapya kila mwaka asilimia
40 ni Vijana wenye umri miaka 15-24"; Alisisitiza Mhe. Mavunde
Aliongeza
kuwa Nchi yetu imeridhia malengo ya
Dunia ya SIFURI TATU ifikapo mwaka 2030, maana yake ni kuwa ifikapo 2030 tuwe
na sifuri ya maambukizo mapya, sifuri ya vifo vitokanavyo na UKIMWI na Sifuri ya vifo vitokanavyo na
UKIMWI,Sifuri ya unyanyapaa na ubaguzi
kwa WAVIU.
Akizungumzia
mwitikio wa wananchi, Mh. Mavunde amesema kuwa anawapongeza Vijana Jijini
Dodoma kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maadhimisho ya wiki ya Vijana
na kushiriki kuzungumzia masuala ya UKIMWI.
Aidha,
Mhe. Mavunde alibainisha kuwa Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI kwa
hapa nchini inasema" PIMA VVU,JITAMBUE, ISHI'' kauli mbiu inatoa msukumo
kwa watanzania kujitokeza kupima VVU kwa hiari baada ya ushauri nasaha.
Tume
ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS)
kwa kushirikina na wadau wanaotekeleza shughuli za Mwitikio wa UKIMWI,
imeratibu maadhimisho ya wiki ya Vijana kuelekea kilelele cha siku ya UKIMWI
Duniani Desemba Mosi 2018 yanayotarajiwa kufanyika Jijini Dodoma.
0 comments:
Post a Comment