Baadhi
ya Wataalamu wa Afya moja wakiwa katika majadiliano wakati
wa mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika kutoa maoni
ya kuandaa sheria ya ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi, Jijini
Dares salaam.
Wataalam wa Afya moja nchini ambao ni wataalam wa sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya
wanyamapori, mifugo, mazingira pamoja na wanasheria wa sekta hizo, wameanza
mchakato wa kuandaa sheria ya kudhibiti athari za vimelea hatarishi kwa jamii,
sheria hiyo itasimamia ulinzi na usalama wa sampuli za vimelea hivyo.
Vimelea
hatarishi vinaweza sambaza magonjwa kwa wanyama na binadamu iwapo ulinzi na
usalama wake hautaimarishwa wakati wa kuvichukua kwa wanyama, binadamu na
mimea au wakati wa kusafirisha vimelea hivyo na kuvipeleka
maabara kwa ajili ya Uchunguzi pia wakati wa kuviharibu mara baada ya
kuvifanyia uchunguzi.
Akiongea
wakati wa mkutano wa Kamati ya Ufundi ya Usalama wa Afya na Ulinzi dhidi
ya vimelea hatarishi vya magonjwa Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Idara ya
Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe amebainisha kuwa
serikali kupitia Dawati la uratibu wa Afya moja lilipo chini ya Ofisi ya
Waziri Mkuu inategemea sana utaalamu wa kamati hiyo kutoa maoni
yatakayojumuishwa katika sheria zitakazo simamia udhibiti wa vimelea hatarishi.
“Serikali itaendelea
kuilinda jamii ya watanzania dhidi ya majanga yanayoweza kusababishwa na
vimelea hatarishi ambavyo husababisha magonjwa ya mlipuko na hatimaye kuleta
majanga kwa jamii, kwa kulitambua hilo Ofisi ya Waziri Mkuu imeamua kuwakutanisha
wataalamu husika ili watoe maoni yao juu ya udhibiti wenye nguvu ya kisheria”
Amesema kanali Matamwe.
Nao
waratibu wa masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi katika wizara ya
Afya na Mifugo Bw. Jacob Lusekelo na Joseph Masambu walibainisha kuwa udhibiti
wa vimelea hatarishi ni muhimu kuwa na nguvu ya sheraia kwani
kumekuwepo na muingilianao mkubwa baina ya nchi
mbalimbali, ambapo muingiliano huo hungeza milipuko ya
magonjwa kwa afya ya binadamu, wanyama
na mimea.
Afya
Moja ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu, wanyamapori, mifugo
na mazingira katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa
yanayoathiri binadamu, wanyamapori na mifugo. Kwa kutambua umuhimu huo
Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana Wizara ya
Afya wameratibu mkutano huo kwa kupata wataalamu kutoka Shirika la
DTRA na Ufadhili wa CDC.
0 comments:
Post a Comment