Wanawake
wengi wanaofanya kazi katika sekta zisizo rasmi hasa maeneno ya viwandani
wamekuwa wakinyanyasika kwa kutogewa haki wanayostahili, mpaka kufikia kuvaa
pampasi wakiwa kazini ili kuweza kukabiliana na changamoto za kimaumbile (wakati
wa hedhi) na hata kujisaidia haja ndogo wakati mwingine na hii inatokana kutopewa
muda wa mapumziko wakiwa kazini.
Muwezeshaji wa semina ya Jinsia na Maendeleo Jackson Masawe akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mapema wiki hii Makao Makuu ya TGNP Mtandao, Mabibo jijini Dar es salaam.
Hayo
yamesemwa mapema wiki hii na Mwanaharakati Jackson Masawe wakati akiongoza
Semina za Jinsia na Maendeleo na mada kuu ikiwa ni kutokomeza ukatili wa kijinsia katika maeneo
ya kazi, na hii ikienda sambamba na kuelekea katika Maadhimisho ya Siku 16 za
kupinga ukatili wa kijinsia Duniani.
Maadhimisho
hayo ambayo ufanyika kila mwaka duniani kote kila ifikapo tarehe 25 mwezi wa
11 na kilele chake kinakuwa ni tarehe 10
ya mwezi wa 12, yenye lengo la kukumbuka matukio kadhaa makubwa yaliyowahi
kutokea duniani ambayo yalidhihilisha ukatili wa kijinsia kwa kiwango kikubwa.
Alisema kuwa
kauli mbiu ya kitaifa kwa mwaka huu inasema “Usalama wake ni wajibu wangu” hii
ikiwa inawalenga waajiri wote kuhakikisha inawajali wafanyakazi wake kwa kuwapa
vitendea kazi na kujali usalama wao wakiwa katika maeneo yao ya kazi.
Aliongeza
kuwa “Sisi kama wana Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) inabidi tufanye kitu
cha tofauti ili kuweza kuleta ukombozi kwa jamii inayonyanyaswa na baadhi ya
watu wachache waliopewa mamlaka ya kuongoza wenzao, ikiwa ni miongoni mwa njia
za kuenzi siku hizi 16 za kupinga ukatili wa kijinsia duniani”. Alisema Jackson
Na baadhi ya
njia zilizopendekezwa na wadau ni kuandaa kongamano kubwa litakalowahusisha
wadau mbalimbali kutoka idara za Serikali, Mashirika binafsi pamoja na kuwaalika
wasimamizi/viongozi wa viwanda mbalimbali ili kuwapa elimu juu ya haki za
wafanyakazi wao na kuwakumbusha wajibu wao kama viongozi.
Lakini pia
njia nyingine ni kuandaa Matembezi ya hiari na kusambaza vipeperushi huku
wahusika wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali za kuhamasisha matajiri
wanaosimamia shughuli mbalimbali ikiwa ni viwandani, Majumbani, Mashuleni hata
Masokoni kujua thamani za wafanyakazi wao.
Na mwisho
washiriki wa semina hiyo walihamasishana Kutembelea vituo vya watoto wenye Ulemavu,
Yatima ili kujua changamoto wanazokutana nazo pamoja na kwenda hospitalini
kujionea ukatili unaofanywa na wauguzi kwa wagonjwa wao.
Mwanaharakati kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Silvia Sosteness akitoa maoni yake katika mjadala wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia katika Maeneo ya Kazi.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia semina kwa umakini.
Semina ikiendelea.
0 comments:
Post a Comment