METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, October 7, 2018

ZAIDI YA WATOTO 1,300 KUSHIRIKI KAMPENI YA KUPINGA VITENDO VYA UKATILI KWA WATOTO WA MIKOANI

 Baadhi ya vijana ambao wanashiriki kampeni hiyo ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya watoto mkoani Iringa zoezi ambalo linaenda sambamba na utoaji elimu ujasiriamali kupitia michezo.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

ZAIDI ya watoto 1,300 wamejuishwa katika kampeni ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya watoto mkoani 



Iringa zoezi ambalo linaenda sambamba na utoaji elimu ujasiriamali kupitia michezo.

Mratibu wa mradi wa kuwawezesha wasichana kiuchumi uliochini ya shirika la BRAC Anna David amewaambia waandishi wa Habari katika viwanja vya chuo kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa (MUCE)  

kuwa lengo la kufanya michezo hiyo kuwaleta pamoja watoto kutoka pande mbalimbali na kuwapa elimu juu ya kupinga ukatili kwa wasichana siku chache kabla ya kufikia maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike yatakayofanyika baadae Octoba 11 mwaka huu katika viwanja vya mwembetogwa mjini Iringa.

Bi David alisema katika maadhimisho hayo Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Salum Hapi anatarajia kuwa mgeni rasmi, maamisho ambayo siku ambayo vilevile ulimwengu unaadhimisha.

Mratibu wa mradi huo alisema waliamua kuijumuisha mkoa wa Iringa baada ya kuona unakabiliwa na visa vya ukatili na hadi sasa wamekwisha kuunda klabu zipatazo 50 ambazo zimekuwa zikitumika kutoa elimu ya kupingana vitendo vya ukatili, ujasiriamali ,kuibua vipaji vya watoto ,kuwafundisha namna ya kuweka fedha na kujiajiri.

Mashindano hayo yameshirikisha watoto wa shule za msingi,sekondari na baadhi ya watoto ambao wameshindwa kuendelea na masomo yao kwa sababu tofauti.

Alisema kuwa kupitia michezo chini ya mwavuli wa shirika lisilo la kiserikali la BRAC wamepeleka zaidi ya watoto 160 chuo cha veta kwa ajaili ya kujifunza ujasiriamali.

Nao baadhi ya washiriki wa michezo hiyo Sarafina Mwinuka alisema kuwa amepata elimu ambayo itamsaidia kuepuka na mambo yasiyofaa ikiwamo usinzi,ndoa na mimba za utotoni.

Naye agetine Joseph na Neema Pius walisema kuwa wanajifunza stadi mbalimbali za maisha ikiwamo kuweka akiba,kujitambua na michezo hiyo imefanyika ikiwa wanaadhimisha siku 16 za kupinga ukatili kwa watoto.


Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com