Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akimsikiliza Balozi wa Australia nchini Alison Charters alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali kuhusu Sekta ya Madini. Wengine ni Mwenyekiti kutoka Tume ya Madini Prof. Idris Kikula na Wataalam kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini na Ubalozi huo.
Na
Asteria Muhozya, Dodoma
Naibu
Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amesema wadau wa Sekta ya Madini Kimataifa
hivi sasa wanaelewa umuhimu wa Tanzania kufanya mabadiliko katika Sekta husika yakiwemo
ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 yaliyofanyika Mwaka 2017.
Naibu
Waziri ameyasema hayo leo ofisini kwake jijini Dodoma alipokutana na Balozi wa
Australia Nchini, Alison Charters ambaye amemtembelea Naibu Waziri Nyongo kwa
lengo la kujadiliana masuala kadhaa katika sekta ya madini ikiwemo kupata
mrejesho wa ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa Madini kwa nchi za Afrika
uliofanyika mwezi Agosti, 2018, nchini Australia, ambapo katika mkutano huo,
Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri Nyongo.
Naibu
Waziri Nyongo amesema kuwa, awali wadau katika mkutano huo walikuwa na uelewa
tofauti lakini mara baada ya kutoa wasilisho kuhusu mabadiliko hayo katika
mkutano huo, waliona umuhimu wa Tanzania kufanya mabadiliko hayo kwa maendeleo
ya nchi na sekta nzima.
“Mhe.
Balozi nashukuru kwa nafasi hiyo isipokuwa nilitamani kupata nafasi zaidi ya
kuelezea uzoefu wetu na mabadiliko katika sekta ya madini,” amesisitiza Naibu
Waziri.
Ameongeza
kuwa, wawekezaji wengi hawana tatizo na mabadiliko ya Sheria ya Madini ya Mwaka
2017 yaliyofanywa isipokuwa changamoto ipo katika kipengele cha chanzo cha
mtaji kutoka katika benki za ndani suala ambalo amesema wizara imelichukua na
inaifanyia kazi.
Pia,
Naibu waziri amemshukuru Balozi Charters kwa kumwezesha kukutana na wadau mbalimbali
wa sekta ya madini wakati akiwa nchini humo, kwani, wadau hao wameonesha nia ya
kuisaidia Tanzania katika masuala ya uongezaji thamani madini nchini na mafunzo
kwa wataalam wa sekta.
“
Tulizungumza masuala mengi na umuhimu wa sisi kuhamasisha shughuli za uongezaji
thamani madini kufanyika hapa nchini. Tunasisitiza suala hili kwa kuwa hivi
sasa tumezuia usafirishaji wa madini ghafi nje ya nchi”, amesema Naibu Waziri
Nyongo.
Kwa
upande wake, Balozi Charter amesema nchi hiyo itaona namna bora ya kufanya ili
kuweza kuisaidia Tanzania kutoa mafunzo kwa wataalam wa sekta husika lengo
likiwa ni kuwajengea uwezo ili waweze kusimamia sekta hiyo vizuri.
“Tunayo
bajeti kidogo lakini tunaweza kufanya jambo kwa ajili ya wizara ya madini
katika utoaji wa mafunzo. Ikiwezekana hata kuwaleta wataalam wetu kuja kutoa
utaalam huo hapa nchini,” amesema Balozi.
Aidha,
Balozi huyo ameeleza kuhusu fursa za masomo ambazo zimekuwa zikitolewa nchini
Australia zikiwemo nafasi za mafunzo ya
muda mrefu na mfupi na hivyo kuwataka wataalam wa Tanzania kuomba nafasi hizo pindi zinapojitokeza.
Pia,
balozi huyo ametaka kujua majukumu ya Tume ya Madini mara baada ya tume hiyo
kuanzishwa ambapo Mwenyekiti wa Tume hiyo ambaye naye amehudhuria kikao hicho,
Profesa Idris Kikula amemweleza balozi huyo majukumu yanayosimamiwa na tume
hiyo ikiwemo mikakati ya tume katika kutatua changamoto zilizopo katika sekta
husika.
Akizungumzia
mabadiliko katika sekta ya madini pamoja na masuala ya uwajibikaji kwa kampuni
za madini kwa jamii, balozi Charter amesema suala hilo ni la msingi kwani hata
katika nchi hiyo masuala hayo yalipewa kipaumbele na kushauri iwapo wizara
inaweza kukutana na wadau kwa ajili ya kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu masuala
hayo.
Mbali
na mrejesho wa ushiriki wa Tanzania katika mkutano masuala ya madini kwa nchi
za Afrika, kikao hicho pia kimejadili masuala ya leseni za madini, Uwajibikaji wa
kampuni za madini katika jamii zinazozunguka migodi na kuhusu kampuni za madini kutumia kampuni za wazawa
kutoa huduma katika migodi.
0 comments:
Post a Comment