Na Munir Shemweta, WANMM
Kilimanjaro
Waziri wa Ardhi Nyumba na
Mandeleo ya Makazi William Lukuvi amewataka watendaji wa sekta ya ardhi nchini
kujisahihisha ili kuepusha mogogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikiwaumuzi wananchi
wengi.
Lukuvi alitoa kauli hiyo jana
alipozungumza na wananchi 97 wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi na Halmashauri
ya Moshi Vijijini katika mkoa wa Kilimanjaro waliojitokeza kwa ajili ya
kuwasilisha kero zao za ardhi kupitia program ya Funguka kwa Waziri.
Alisema, ni vyema katika
kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya tano watendaji wa sekta ya ardhi wakaanza
kujisahihisha ikiwemo kuweka majalada yote ya ardhi vizuri kabla hajatembelea
maeneo yao kinyume chake atawashughulikia wote watakaobainika kukaidi ama
kutoweka sawa majalada ya ardhi.
“Mtu yeyote anayetaka kuingusha
Serikali katika masuala ya ardhi tutamuangusha yeye na lazima tutekeleze ilani
ya Chama cha Mapinduzi kwa vitendo” alisema Lukuvi.
Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Serikali itawanyoosha wale wote wanaoenda
kinyume na maadili ya utumishi na kubainisha kuwa hata wale watendaji wa ardhi
walioharibu huko nyuma watashughulikiwa.
Akigeukia migogoro ya ardhi,
Lukuvi alisema migogoro mingi inayojitokeza sasa ni ile ya miaka ya nyuma ya
kuanzia miaka ya themanini na kubainisha kuwa kupungua kwa migogoro mipya
kunatokana na Serikali ya sasa kuweka mazingira mazuri ya kushughulikia masuala
ya ardhi.
“Leo watendaji wa sekta ya
ardhi wamenyooka na kazi ya serikali ya awamu ya tano ni kuwanyoosha wale
wanaoenda kinyume na taratibu na sheria katika kushughulikia masuala ya ardhi.
Akigeukia suala la wamiliki wa
ardhi kuchukuliwa maeneo yao bila kulipwa fidia, Lukuvi amewahakikishia
wananchi waliohudhuria mkutano huo kuwa, Serikali inalipa kipaumbele suala la
fidia kwa wale ambao maeneo yao yatachukuliwa.
Aliwaeleza kuwa hata ikitokea
mtu hakufidiwa kipindi ambacho eneo lake limechukuliwa lakini malipo yake
yataanza kuhesebiwa pale eneo lilipochukuliwa na kiwango cha fidia kitakuwa
kikiongezeka kadiri malipo yake yanavyochelewa.
Pia aliwaeleza wananchi
waliokusanyika katika ukumbi wa ofisi wa mkoa wa Kilimanjaro kuwa wale wote
ambao maeneo yao yalishatolewa maamuzi na Mahakama hakuna mtu yoyote mwenye
mamlaka ya kubatilisha ikiwemo Serikali.
0 comments:
Post a Comment