Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mamia ya wakulima leo tarehe 3 Octoba 2018 katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati akimuwakilisha Rais, John Pombe magufuli katika Maadhimisho ya Miaka 25 ya Mtandao wa wakulima Tanzania (MVIWATA), (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mamia ya wakulima leo tarehe 3 Octoba 2018 katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati akimuwakilisha Rais, John Pombe magufuli katika Maadhimisho ya Miaka 25 ya Mtandao wa wakulima Tanzania (MVIWATA),
Mamia ya wakulima wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumzaleo tarehe 3 Octoba 2018 katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati akimuwakilisha Rais, John Pombe magufuli katika Maadhimisho ya Miaka 25 ya Mtandao wa wakulima Tanzania (MVIWATA).
Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa mkulima wa uyoga, Maria Shindika wa Mvomero
(kulia) kabla ya kuhutubia katika Maadhidhimisho ya Miaka 25
ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima (MVIWATA) yaliyofanyika
kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Oktoba 3, 2018.
*Asema
zaidi ya wakulima wadogo 527,000 katika
Mikoa 13 wamenufaika
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetoa mikopo yenye
thamani ya sh. bilioni 56.45 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kilimo
katika mikoa 13 hapa nchini.
Amesema mikopo hiyo imetolewa katika kipindi cha
kuanzia Agosti 2015 hadi Septemba 2018, kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB).
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Oktoba 3,
2018) kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima
Tanzania (MVIWATA) mjini Mororogo.
Mikopo hiyo
imewanufaisha wakulima wadogo zaidi ya 527,000 waliopo kwenye mnyororo wa
thamani wa mazao ya kahawa, karafuu, mahindi, mbogamboga na mazao mengine.
Amesema Serikali inatekeleza mipango mbalimbali kwa lengo la
kutatua kero zinazowakabili na kuwawezesha wakulima wadogo kujikwamua kiuchumi
kupitia kilimo.
Amesema Juni 14, mwaka huu Rais Dkt. John Magufuli, alizindua
Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo hapa nchini (ASDP II) yenye lengo
la kuboresha sekta ya kilimo.
Waziri Mkuu amesema ASDP II inalenga kuhakikisha sekta ya kilimo
inapewa kipaumbele stahiki ili iweze kuleta tija kwa wakulima wenyewe na Taifa
kwa ujumla.
“Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha sekta
ya kilimo ikiwemo kutoa mikopo kwa wakulima wadogo; kuondoa baadhi ya tozo
zenye kufifisha uzalishaji.”
Pia kuweka mipango mizuri ya matumizi bora ya ardhi na kutafuta
masoko pamoja na kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo ili kumuongezea tija
mkulima.
Kadhalika, Waziri Mkuu ameongeza kuwa mchango wa wakulima wadogo
umewezesha Taifa kujitosheleza kwa chakula na hata kuuza nje ya nchi mazao ya
kilimo.
Hivyo, Waziri Mkuu ametoa rai kwa viongozi na watendaji wa
Serikali kujenga utamaduni wa kuhudhuria wa kukutana na kuzungumza na wakulima
kuhusu mahitaji hayo.
“Tunafahamu kwamba wakulima mna changamoto nyingi zikiwemo za
kisera, kirasilimali na kiutendaji kwenye masuala ya ardhi, masoko, mitaji na
hata kero za tozo na ushuru.”
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameagiza Wakala wa Vipimo nchini
(WMA) waendesha msako utakaowanasa wafanyabiashara wanaowaibia
wakulima kwa njia ya udanganyifu wa kutumia vipimo
visivyo sahihi.
Waziri Mkuu amesema mfanyabiashara yeyote atakayebainika kuwaibia
wakulima kwa kutumia vipimo visivyo rasmi achukuliwe hatua za
kisheria.
“Utaratibu wa kutumia vipimo visivyo rasmi ambavyo
vimepewa majina ya lumbesa, kangomba, umejileta mwenyewe na
mengine mengi lazima ukomeshwe.”
Waziri
Mkuu ameuagiza uongozi wa WMA kwa kushirikiana na halmashauri zote
nchini wahakikishe mazao ya wakulima yanauzwa kwa kutumia vipimo rasmi ili
wasiendelee kupunjwa.
Akizungumzia kuhusu kero
ya ardhi, Waziri Mkuu amesema Serikali itawapa
wananchi ardhi inayotwaliwa kutoka kwa wawekezaji au
wamiliki walioshidwa kukidhi masharti na yale yasiyoendelezwa kwa
muda mrefu.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 – Dodoma
JUMATANO, OKTOBA 3, 2018.
0 comments:
Post a Comment