Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim
Wangabo amewaagiza wakurugenzi kushirikiana na madiwani kuhakikisha suala la
kupunguza udumavu katika mkoa wa Rukwa linakuwa ni ajenda ya kudumu katika
vikao vya mabaraza ya madiwani pamoja na mikutano ya hadhara katika
kuwaeleimisha wananchi juu ya athari ya udumavu.
Amesema kuwa suala la udumavu
lisisahaulike pindi tunapoangalia ufaulu wa watoto wetu mashuleni, na kuwa
mstari wa mbele kutoa ahadi za kuhakikisha watoto wanaongeza ufaulu huku
udumavu ukiwa bado haujashughulikiwa.
“Tuone kwamba kama huna hali mbaya ya
matokeo ya kielimu yanachangiwa pia na udumavu kwasababu udumavu umekuwa wa
muda mrefu na kama tunaukubali upo, sasa kwanini usikubaliane pia na matokeo
yanayotokea, tuweke jitihada kubwa sana kuondoa udumavu ili watoto wetu
waongeze ufaulu,” Alisisitiza.
Ameongeza kuwa kama si hivyo basi
itabidi takwimu udumavu ziangaliwe upya, ama kama kwenye elimu kuna kupasi sana
basi kuna wizi wa mitihani ama kuna wageni wengi sana wanaotoka nje kuja kusoma
Kwetu.
Mwanzoni mwa mweze wa nane Mh. Wangabo
aliingia mkataba wa utendaji kazi na kusimamia shughuli za lishe baina ya Ofisi
yake pamoja na wakuu wa wilaya ambapo ni utekelezaji wa maagizo ya Wizara ya
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mikoa juu ya kupunguza
utapiamlo ambao kitaifa ni asilimia 34.
Kwa upande wake mganga Mkuu wa mkoa wa
Rukwa Dkt. Boniface Kasululu alisema kuwa utapiamlo unasababisha udumavu wa
akili na mwili na ubongo wa mtoto unaendelea kukua tangu ujauzito mpaka
anapofikisha miaka mitano.
“Wananchi
wengi hawana uelewa wa kutosha juu ya masuala ya lishe bora na athari za
utapiamlo. Pamoja na kuwa Mkoa unazalisha vyakula vya aina mbalimbali
tena kwa wingi, lakini wananchi wengi bado wanatumia aina moja au aina za
vyakula vilivyozoeleka kwa muda mrefu bila kuchanganya na aina nyingine za
vyakula ili kufikia mahitaji halisi ya virutubishi.” Alisema.
Mkoa wa
Rukwa una kiwango cha utapiamlo cha asilimia 56.3 wakati kitaifa ni asilimia
nne, na kitaifa mkoa wa rukwa umeshika nafasi ya 19 mwak huu tofauti na mwaka
jana ulikuwa wa 15 kitaifa katika matokeo ya darasa la saba.
0 comments:
Post a Comment