Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akitolea
ufafanuzi juu ya swala la tatizo la umeme mara baada ya kupigia simu meneja wa
tanesco wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Wananchi wa kata ya Rungemba mkoani Iringa wamemuweka kikaangoni
mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi juu ya kukosekana kwa umeme
katika baadhi ya vitongiji ya kata hiyo.
Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara wananchio hao wamesema kuwa
wamekuwa walinzi wa umeme ambao umepita katika kijiji cha Rungemba.
“Sisi watu wa Makwawa na Njia Panda tumekuwa walinzi wa huu umeme
ambao umepita kwenye hiki kijiji cha Rungemba na kata kwa ujumla maana hakuna
hata laini ndogo ambayo inasemekana imepita lakini tumekuwa tunashangaa maana
hakuna hata hiyo laini” walisema wananchi hao
Wananchi hao wameendelea kwa kusema kuwa umeme huo toka umefika
hauna faida kwa wananchi wa kijiji hicho kwa kuwa wamepelekewa transifoma yenye
nguvu ndogo kulingana na mahitaji ya wananchi.
“Tumewekewa transifoma haina uwezo kwa kuwa inashindwa hata
kusukuma mashine za kusagia mahindi hivyo inatulazimu kusafiri zaidi ya
kilometa saba kwa bodaboda kupata huduma ya kusaga mahindi” alisema wananchi
Aidha wananchi hao wamesema kuwa wapo tayari kulipia nguzo za
umeme ili waweze kupata nishati hiyo kwa maendeleo ya wananchi na kijiji hicho.
Naye mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akaamua
kumpigia simu meneja wa tanesco wilaya ya Mufindi Omary Ally kupata ufumbuzi wa
tatizo hilo mbele ya wananchi.
“Meneja nimebanwa hapa kwenye mkutano wa hadhara na wananchi juu
ya tatizo la umeme hapa Rungemba hali ipoje” aliuliza swali kwa meneja?
Akijibu hoja hizo meneja wa Tanesco wilaya ya Mufindi Omary Ally
kuwa kulikuwa kunatatizo la transifoma hiyo baada ya wiki moja watafunga na
wananchi watapata nishati ya umeme ya uhakika kabisa
Hata hivyo Ally akawatoa hofu wananchi kwa kuwaahidi kuletea
transiafoma ambayo itakidhi mahitaji ya wananchi wa kijiji hicho na kuondokana
na kero hiyo ambayo inarudisha nyuma maendeleo.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya wananchi kata ya Rungemba kukaa
kwa kipindi cha muda mrefu bila kuwa na huduma hiyo ya umeme.
0 comments:
Post a Comment