Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akikagua mfereji wa maji wa Mkombozi na Mboliboli Tarafa ya Pawaga Mkoani Iringa kwa ajili ya umwagiliaji wa mashamba ya mpunga katika ziara ya kikazi ya kukagua hali ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya Nyanda za juu kusini Jana tarehe 12 Octoba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akikagua mashamba ya mpunga alipotembelea Tarafa ya Pawaga Mkoani Iringa katika ziara ya kikazi ya kukagua hali ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya Nyanda za juu kusini jana tarehe 12 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba
akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela akiwa katika
ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Iringa kukagua hali ya upatikanaji wa
mbolea kuelekea msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019.
Na
Mathias Canal-WK, Iringa
Waziri wa
Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba amewaagiza wataalamu wa umwagiliaji kuzuru
Tarafa ya Pawaga ili kutembelea na kukagua mfereji wa maji wa Mkombozi na
Mboliboli Tarafa ya Pawaga ili kuanzisha skimu ya umwagiliaji.
Waziri Tizeba
ametoa agizo hilo Jana tarehe 13 Octoba 2018 wakati alipotembela eneo
la mashamba ya mpunga wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili
Mkoani Iringa ya kukagua hali ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya Nyanda
za juu kusini.
Alisema kuwa
mfereji huo unaohudumia wakulima wa mpunga katika vijiji vya mboliboli,
Usolanga, Mbugani na Mkumbwani unapaswa kuwekewa mkakati wa haraka ili kujengwa
skimu ya umwagiliaji kwa ajili ya mashamba ya wakulima yanayotajwa kuwa na
ukubwa wa hekari 11,000.
"Kwa
bahati nzuri Tume ya umwagiliaji sasa rasmi imehamishiwa kwangu haina hata siku
tano nitawasimamia kweli kweli ili kuwa na matokeo makubwa na ya haraka kwenye
kilimo ambacho ndicho mkombozi wa mkulima" Alikaririwa Dkt Tizeba
Aidha,
aliwashauri wakulima katika Tarafa hiyo ya Pawaga kuingia katika kilimo cha
pamoja ili pindi wanapovuna waweza kuuza kwa pamoja jambo litakalowafanya kuwa
na maamuzi ya kupanga bei waitakayo ya Mazao.
Waziri Tizeba
ameitaka Tume ya umwagiliaji kufanya uhakiki wa maeneo yote ya mashamba hayo ya
wakulima kwa kuyapima kabla ya kuingia katika kilimo cha pamoja ikiwa ni pamoja
na kuainisha gharama za ukamilifu wa mfereji huo wa Mkombozi na Mboliboli.
Alisema kuwa
faida ya kulima kwa pamoja wakulima wanapata fursa ya kukopeshwa kirahisi na
Mabenki kuliko kufanya kuomba mkopo kwa mkulima mmoja mmoja kwani masharti yake
yanakuwa magumu zaidi.
Kadhalika,
Waziri Tizeba amemuagiza Mshauri wa Kilimo wa Mkoa wa Iringa Bi Grace Macha
kuanisha uhitaji wa mbegu katika Mkoa huo ili taarifa zitolewe haraka kwa
Wakala wa Taifa wa Mbegu (ASA) ili waweze kutoa mbegu punde msimu unapoanza.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment