METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, September 17, 2018

GWAJIMA AMSHAURI LOWASA KUSTAAFU SIASA ILI KULINDA HESHIMA YAKE

Kada wa CCM Ndugu Methusela Gwajima, amemshauri Waziri mkuu mstaafu wa Tanzania, Mheshimiwa Edward Lowasa Kustaafu rasmi harakati zake za kisiasa na hasa siasa za majukwaa ili kulinda heshima yake.

Gwajima amesema ,Kipigo cha Monduli alichopata ni kibaya mno na ni zaidi ya Kipigo Cha Mbwa Koko kiasi  kwamba, kisiasa sasa anatia aibu/Huruma/Simanzi, hivyo anapaswa kusoma  alama za nyakati  kwani kama ni kuisoma namba  hakika hii ya Monduli ni ya kufunga  mwaka !!

“Hivi kweli  kama umeweza kushindwa kulikomboa Jimbo moja tu  tena la Nyumbani kwako, Je utaweza tena kuhimili mchaka mchaka wa  nchi nzima ? Kwa hakika busara ya kawaida inakutaka upumzike na ikibidi uachane kabisa na harakati za kisiasa, baki nyumbani  walau hata uwe  mshauri tu kwa watu watakaohitaji ushauri wako” alisema Gwajima.

Gwajima ambaye ni Mwanasheria kitaaluma amemtaka Lowasa Kuepukana na washauri wabaya waliomzunguka kwani  kwa mara nyingine tena wamefanikiwa kumuingiza  chaka  bure mzee wa watu.

“Nadhani, Mhe. Lowasa amezungukwa na genge la wahuni  na wapiga dili ndio maana wanashindwa kumpatia ushauri mzuri unaoendana na umri na heshima yake.

Mhe. Gwajima amewapongeza wagombea wote wa CCM waliofanikiwa kupata ushindi  wa  kishindo “Hongera sana wanaukonga, Hongera sana wana Monduli, Hakika nyinyi hampangiwi cha kufanya ama kweli wanaukonga na  Monnduli sio wa mchezo  mchezo”

Mhe. Gwajima  amevipongeza  vyombo vyote vya dora kwa kusimamia amani na utulivu wakati wote wa kampeni na hatimaye katika zoezi  zima la uchaguzi.

Ushindi huu wa CCM   katika chaguzi ndogo zilizofanyika jana ,ni ishara kubwa ya imani walionayo wananchi kwa serikali yao chini ya Mhe. Raisi wetu Mpendwa Dr. John  Pombe  Magufuli katika kusimamia utekelezaji  wa ilani ya chama cha mapinduzi.

Mhe. Gwajima amepongeza  Mh. Raisi  Magufuli kwa kufanya mambo makubwa ya wakuwaletea wananchi maendeleo katika sekta zote na mda mfupi sana tangu aingie madarakani.

Mhe. Gwajima Alimpongeza Rais Magufuli kwa ujasiri wake na usimamizi katika kusimamia Ujenzi wa Bomba la mafuta HOIMA –TANGA, Ongezeko Katika makusanyo ya kodi –TRA, Mradi wa STIEGLERS’S GORGE MEGAWATI  - 2,100, Mahakama wa rushwa na uhujumu  uchumi na Serikali kuhamia makao makuu DODOMA.

Mafanikio ya kuhusu Elimu bure kuanzia msingi hadi kidato cha nne, Ujenzi wa Ukuta wa kulinda Madini MERERANI, Kufufua Shirika la ndege nchini, Usajili wa kuwatambua rasmi wamachinga 20,000, Huduma  bora za tiba kwa watanzania na Mafanikio makubwa katika ujenzi wa miundombinu mfano mzuri ni Flying Over ya Tazara.

Mwisho Mh. GWAJIMA amewaomba watanzania kuendelea kumuunga mkono Raid Magufuli.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com